Majadiliano:Mtaguso Mkuu
Ihamishwe
haririMakala hii inasimama upande wa kanisa katoliki. Habari juu ya msimamo wa kiprotestant haziridhishi. Sijajaribu kuibadilisha kwa sababu sipendi magongano naona tuelewane kwanza. Pendekezo langu nimeweka chini ya Mitaguso ya kiekumene. Ikae hivi kwa muda kidogo hadi Riccardo na wengine wanopenda wameangalia yaliyomo. --Kipala (majadiliano) 21:05, 16 Novemba 2008 (UTC)
Ndugu Kipala, asante sana. Nitaangalia kwa makini siku nyingine nitakapokuwa na nafasi zaidi. Kwa leo nasema hivi kwa jumla: 1. Nadhani unaniona kidogo kama kwazo kwako na kwa wiki. Pole. 2. Duniani mtu moja kati ya sita ni Mkatoliki. Kuwaelewa vizuri ni muhimu. 3. Kanisa Katoliki lina historia ndefu yenye matunda mengi: nusu ya sanaa zinazoheshimiwa na Umoja wa Mataifa inahusiana nalo. 4. Uprotestanti wenyewe ni mtoto wa Ukatoliki: haueleweki peke yake. 5. Ugumu wa kueleza msimamo wa Waprotestanti ni kwamba ni tofauti mno. Mlutheri anaweza kuwa karibu na Mkatoliki kuliko alivyo kwa Mprotestanti wa madhehebu kadhaa ya Kimarekani. 6. Msimamo huo unaweza kuyumba kadiri msomaji anavyoelewa Biblia. K.mf. anaweza akakubali uaskofu kwa wanawake au kuwakataza hata wasisome kanisani. 7. Pamoja na hayo ni lazima tujaribu vilevile kuonyesha misimamo hiyo. Ukieieleza wewe ni afadhali kuliko nikijaribu kufanya hivyo mimi. Tutazidi kuelekezana kwa amani! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:53, 23 Novemba 2008 (UTC)
- Riccardo mpendwa, sentensi yako ya mwisho nimependa. Kuhusu na. #1 ninaomba uelewe ya kwamba upande wangu si kweli. Najisikia afadhali kama tunaweza kujadili tofauti ya maoni kwa amani na bila kuona nia mbaya upande mwingine. Hivyo ndivyo inavyotakiwa tukitaka kujenga wikipedia hii. Wewe ni mtu mwenye elimu nzuri na unaweza kutoa michango ya maana! Basi nitasubiri hadi umepata muda kusoma! Ndimi wako --Kipala (majadiliano) 07:51, 23 Novemba 2008 (UTC)