Majadiliano:Mzunguko wa Bahari Nyekundu

Latest comment: miaka 9 iliyopita by Kipala

Periplus ni neno la kilatini ambalo haliendani na sarufi ya kiswahili. Kwa vile katika kiswahili hakuna tafsiri ya moja kwa moja ya neno periplus basi ni vizuri kulitohoa na kuliweka katika sarufi ya kiswahili. Peripulu ndio neno ambalo linakwenda sambamba na sarufi ya kiswahili na pia kulingana na neno la asili katika lugha zilizotumika mwanzo

Mpendwa, Periplus περίπλους si neno la Kilatini bali la Kigiriki cha Kale. Makala inasema vile. Tafsiri yake lipo ni "kuhusu safari (ya baharini)" kwa maana "mwongozo". Sasa inatumiwa kama jina maana hata Kiingereza haina tafsiri ya "moja kwa moja" maana "about sailing" ni tafsiri kamili lakini haieleweki kirahisi. Ukitazama makala za Periplus katika wikipedia za lugha mbalimbali utaona karibu zote zimetumia neno la Kigiriki kama jina. Na kuhusu majina ya kigeni tunajaribu kuyatumia jinsi yalivyo kama hakuna historia ya jina hili kwa Kiswahili. Maanake inaeleweka ya kwamba "Ufaransa, Uingereza, Marekani" ni nchi zipi na maumbo haya ya jina yametokea katika historia. Lakini jina linalojulikana leo tu kwa Waswahili "Elvis Presley" ni Elvis Presley, hatumbadilishi kuwa "Elivisi Pereseli" ingawa umbo kama hili lingelingana zaidi na kanuni za matamshi ya Kiswahili. Naomba utafakari kama una sababu nzuri zaidi , kama ziko ulete!, menginevyo nitarudisha mabadiliko yako. Kipala (majadiliano) 07:02, 14 Januari 2015 (UTC)PReply
Rudi kwenye ukurasa wa " Mzunguko wa Bahari Nyekundu ".