Majadiliano:Ndui ya nyani

Latest comment: mwaka 1 uliopita by ChriKo in topic Tafsiri ya monkeypox

Tafsiri ya monkeypox hariri

Uganda knuckles salaam. Je, ndui ya nyani ndiyo jina rasmi la monkeypox? Ikiwa sivyo, mbona basi umechagua jina hili? Maana ya nyani ni baboon. Jina la jumla la monkey ni kima. Kwa hivyo tafsiri bora ya monkeypox itakuwa ndui ya kima. Tafadhali jibu maoni yangu. La sivyo, nitabadilisha kichwa cha makala haya. ChriKo (majadiliano) 07:40, 4 Juni 2022 (UTC)Reply

Ndugu ChriKo, natumaini unazidi kupata nafuu. Kuhusu jina hilo nililitafsiri mimi badala ya tumbili alilolitumia huyo Uganda knuckles. Kumbe wewe mtaalamu unapendelea kima. Sina la kupinga, isipokuwa kwamba katika matumizi ya wengi neno nyani linatumika zaidi... Sijaangalia kuhusu ndui yao. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:51, 4 Juni 2022 (UTC)Reply
Ndiyo ndugu Riccardo, nimepata nafuu, lakini sijafika 100%. Asante kwa jibu lako. Kumbe, watu huita small tree monkeys nyani pia? Kwa vyovyote vile, ikiwa nyani ni jina la kawaida, basi ugonjwa huo uitwe ndui ya nyani. Amani kwako. ChriKo (majadiliano) 08:38, 4 Juni 2022 (UTC)Reply
Naona sasa mtandaoni jina Homa ya Nyani. Sijui kama ni sahihi zaidi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:03, 4 Juni 2022 (UTC)Reply
Sipendi jina Homa. Siyo sahihi. Jina ndui linaonyesha ni mradhi gani. ChriKo (majadiliano) 09:22, 4 Juni 2022 (UTC)Reply
Return to "Ndui ya nyani" page.