Majadiliano:Pango (kodi)
Latest comment: miaka 6 iliyopita by Riccardo Riccioni
Sidhani kwamba jina pango lafaa kutumika kumaanisha kodi ya nyumba. Nilipoona jina hili katika wikipedia hii nilimaka sana na kuuliza walimu wengi wa kiswahili. Kodi ya nyumba huitwa malipo ya kupangisha maana huwa kuna mpango kati ya mpangaji na mwenye nyumba. Hili jina kupanga latokana na ule mpango.
Nomimo pango lina maana tofauti kabisa. Lamaanisha mahala anapokaa nyoka au wanyama pori wanaokaa kwa cave--JanetKihumba (majadiliano) 12:49, 10 Oktoba 2018 (UTC)
- Dada, labda kwenu Kenya neno hilo halitumiki kwa maana ya kodi, lakini Tanzania ni la kawaida na lipo katika kamusi, kwa mfano Kamusi Kuu ya Kiswahili. Kwa maana nyingine kuna ukurasa pango (jiolojia). Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:27, 10 Oktoba 2018 (UTC)
- Hili la pango(jiolojia) nalijua vizuri na sina wasiwasi nalo. Lile ambalo nina atiati ni hili la pango kama 'rent'. Je, huenda likawa likitumika na Watanzania wenye lafudhi fulani? Huenda likawa ni msimu? Nayauliza haya maana nimeangalia filamu chache za Tanzania na ni kana kwamba wao watumia neno kodi tu au malipo ya kupangisha nyumba. Nitaufanya utafiti zaidi--JanetKihumba (majadiliano) 14:50, 12 Oktoba 2018 (UTC)
- Dada, usihangaike mno: tazama kamusi nyingine pia, kama Kamusi ya Kiswahili Sanifu na Kamusi ya Karne ya 21 ambayo ni kutoka Kenya. Tena hilo lisikufanye ukate tamaa. Michango yako ni mizuri. Amani kwako. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:39, 13 Oktoba 2018 (UTC)