Majadiliano:Sherehe

Latest comment: miaka 7 iliyopita by Muddyb Blast Producer

Labda hizi makala ziwe mbili. Hapa imetaja Ukatoliki tupu wakati sherehe zinafanywa na madhehebu yote na dini zote. Hujaitendea haki.. Weka mafungu mbalimbali ili ipate kuleta maana halisi ya sherehe. Je, sherehe za maadhimisho ya Uhuru? Nawaza tu..--MwanaharakatiLonga 11:36, 18 Juni 2016 (UTC) Reply

Tazama hii:
sherehe1* nm [i-/zi-] celebration,

festival. (Kar)

- labda makala hii iwe sherehe (Katoliki) ili makala ya sherehe ya jumla ijitegemee. Again, naendelea kuwaza tu!

Ndugu, ni kweli kwamba kwa sasa ukurasa unahusu zaidi liturujia ya Kikatoliki, kama ilivyo kwa kurasa za Kiingereza na lugha nyingine. Lakini hakuna shida kama mtu anataka kuongeza humohumo habari za dini na utamaduni wowote. Amani kwa wote! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 04:39, 19 Juni 2016 (UTC)Reply
Itakuwa haina maana iliyokusudiwa. Ndugu, wikipedia ni kamusi elezo ambayo lengo kuu watu wajifunze. Ukiandika makala kwa sherehe za kawaida ambazo si za kidini itapotea maana. Kwa kuthibitisha hilo. Angalia kiungo chake cha interwiki kwenda Kiingereza si sherehe kama sherehe, yaani, celebration au festival. Utaungaje kutoka Kiingereza? Ndiyo maana nikakwambia hapa aidha uweke sherehe "MAANA" kisha upambanue mule.. Ili tupate viungo vinavyojibeba kimantiki. Sijui kama umenipata hapo?--MwanaharakatiLonga 07:02, 19 Juni 2016 (UTC)Reply
Return to "Sherehe" page.