Majadiliano:Tarakilishi

(Elekezwa kutoka Majadiliano:Tarakishi)
Latest comment: miaka 17 iliyopita by Muddyb Blast Producer in topic Kiswahili cha Kompyuta

Karibu na makala yako ya kwanza - na pole kupata ushauri ambao labda haufurahishi mara moja. Naomba angalia http://sw.wikipedia.org/wiki/Talk:Mwanzo#Kiswahili cha Microsoft ! Uko huru kuendelea utakavyo. Tuko wachache kiasi cha kwamba tusivutane kama moja wetu anaandika kwa namna yake - baada ya kupita makala 1000 tuanze kupigana "vita ya wahariri"! Lakini kama orodha ya Microsoft ina umuhimu - basi labda kazi yetu inaweza kuwa bure tusipojali... --Kipala 20:45, 15 May 2006 (UTC)

Tukitukuze kiswahili ipasavo

hariri

Nakushukuru Bw. Kipala kwa kumbusho muhimu kama hili. Naelewa barabara umuhimu wa kuwa na uwiyano wa maneno katika lugha. Kwa kweli nimekua nikitafuta makala kama hii kwa muda mrefu sana, nakushukuru tena.--Mudux01 21:38, 15 May 2006 (UTC)

Kiswahili cha Kompyuta

hariri

Kwanza ni mshangao mkubwa sana kwa kompyuta kuwa na kiswahili chake. Si kitu sana. Zamani kidogo nilikuwa naangalia filamu ya Safari iliotungwa na Tuesday Kihangala kulikuwa na wanafunzi wanasoma huku wakijadili juu ya masuala ya kompyuta mfano: kompyuta wao waliita "Kinakilishi" kwenye wikipedia nikakuta TARAKISHI sasa hapo kidogo nashinwa kuelewa nani mkweli je wewe unaonaje?--Muddyb 14:08, 25 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Hapa ni yale niliyosema. Wakati kitu ni kipya maneno hutafutwa. Ugumu upo hasa kama mwanzoni ni watu wachache wanaotumia kitu kile au kujua habari zake AU pia ni wachache tu wanaoongelea habari zake kwa lugha. Tarakishi/tarakilishi nimekuta hapa nisipokosei lakini kama hakuna mtu huko TZ anayekumbuka neno basi limekufa tayari na sisi tulizike. Tuhamishe makala kwa neno lingine. Lipi? Kompyuta - bila shaka inaeleweka. Kwa upande mwingine ni vizuri kutumia maneno ya kienyeji kama yapo na kama yanafaa na kama yanaeleweka (=masharti matatu).
Naomba andika tu yale unayojua hapa bila kujali jinsi ilivyoandikwa sasa! --Kipala 14:23, 25 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Sawa lakini ipo njia rahisi nafikiri. Nitafuta siku nimuone yule mtangazaji wa kipindi anitajie maneno yote au nisubiri siku ya kipindi kisha wao hutoa barua pepe yao nitaiandika kisha nitatuma maswali yangu yote. Chamsingi ni kuwafuta tu na kuwauliza juu ya lugha inayotumika kutajia vifaa vya kompyuta ili tuweze kuwa sawa je waonaje nifunge safari ya hiyo?--Mwanaharakati 14:39, 25 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Hii ni hoja zuri na la maana sana. Labda waulize kama wanatumia orodha ya maneno ya KILINUX ya UDSM au wafanyeje? Asante! --Kipala 14:42, 25 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Wale watu wanaonekana ni wajuzi hasa manake hata kiswahili chao ni cha hali ya juu sana. Hawazungumzi kwa kubabaisha wanajiamini kwamba yale wanayosema ni sahihi kabisa. Kuna ulazima wa kuonana nao wale watu. Tafadhali tukumbushane ukiona imefika jumamosi basi nikumbushe ili niweze kwenda kwa siku ya Jumapili. Naona mwanzo uliona kulikuwa kimya sana. Nilikuwa narekebisha makala ya Kong'oli. je unaweza kusoma hii makala na uniambie umeelewa nini.--Mwanaharakati 14:47, 25 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Rudi kwenye ukurasa wa " Tarakilishi ".