Majadiliano:Usawa (hisabati)

Latest comment: siku 1 iliyopita by Riccardo Riccioni in topic Usawa

Usawa

hariri

@Riccardo Riccioni Mambo vipi? Jina la makala hii ni "Usawa". Lakini, makala inahusu dhana ya namba shufwa na namba witiri, ambayo ni tofauti na dhana ya namba iliyo sawa na namba nyingine. Inaonekana tafsiri sisisi ya "parity" katika Kiingereza. Naamini kwamba "Namba shufwa na witiri" au hata "Ushufwa" ingekuwa jina lifaalo zaidi. Kisare (majadiliano) 05:45, 19 Desemba 2024 (UTC)Reply

@Kisare. Asante kwa kunishirikisha. Mimi nilichangia makala hiyo mara moja tu mwaka 2015. Naona wazo kuu ni "usawa wa kudumu wa idadi ya namba shufwa na zile witiri", ila kichwa hicho ni kirefu mno. Usawa ni kifupi kiasi kwamba kinaweza kisieleweke. Labda "Idadi sare ya shufwa na witiri"? Amani kwako. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:33, 19 Desemba 2024 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Usawa (hisabati) ".