Majadiliano:Utatu
Latest comment: miaka 4 iliyopita by Kipala
Mbona hiyo haipatani na akili iweje yehova awe nafsi tatu?
- Ndugu, si suala la akili ya kibinadamu, ila la kumuamini Mungu alivyojifunua. Yesu ametuagiza tubatize kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Jina moja kwa watatu. Kwa vyovyote Wikipedia inaeleza imani ya watu bila ya kutetea wala kupinga kwa hoja. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:18, 20 Desemba 2019 (UTC)
- Ilahali tunaruhusiwa kujadiliana kwenye kurasa za majadiliano: jibu la swali lako linategemea kiwango cha akili. Ukiwa na elimu (tofauti na akili) unaweza kujua "Yehova" (heri kwa Y kubwa ukitaka kuandika Kiswahili) si jina, ni kosa la kusoma jina la Kiebrania la Mungu. Kwa akili yako: ukiwa na kiuu na kuniomba nikupe maji, utasemaji nikikupatia kipande cha barafu cha kilo tano? Nahofia hutapenda kuishika. Vilevile hutapenda nikukupa lita ya maji kwa umbo la mvuke la °C 100. Kumbe, yote maji. Inapatana na akili yako? Kipala (majadiliano) 10:04, 21 Desemba 2019 (UTC)