Majadiliano:Wawanji

Latest comment: mwezi 1 uliopita by EDICKO STANLEY in topic Wawanji

katika makala ya kabila la wawanji kudhaniwa asili yao ni Dodoma kwa majina mfano Ngogo huyu alikuwa ni mgogo kwa kabila alipofika uwanji utamkwa hiyji wa neno mgogo ikawa "N'gogo" yaani mgogo huyu maendeleo ya lugha na maingilio ya lugha za kigeni wakashindwa kutamka N'gogo wakaondoa alama ' ikaunganishwa na kuwa Ngogo.

lakini kwa majina kama msemwa mkinda sidhani kama yana ithbati sana kwani utawakuta nkinda usukumani, mara na pia utawakuta msemwa wabena hivyo utafiti zaidi ufanyike

Wawanji

hariri

mimi pia ni muwanji wa ukoo wa NGUVILA ukoo wetu kwa sehemu kubwa tupo vijiji vya matamba na nhungu, japo sijakulia uwanji, ila nimewahikusoma historia kwa ufupi nikiwa mdogo sana kati ya darasa la nne au la tano nilisoma katika Moja ya vitabu alivyokuwa navyo baba kuhusu historia ya ukoo wetu maana pia tulikuwa ukoo wa kichifu ambapo chifu wa mwisho kwetu alikuwa ni Babu yake na baba mzee Sakalani, ambao jina maarufu la ukoo wetu ni NGUVILA Mwaulesi(mwabhulesi)

Historia Ile ilikuwa inaanzia ubenani ambako NGUVILA halisi yaani vizazi vya nyuma sana huko, alikuwa mtumwa kwenye mashamba ya ulezi ya wakoloni na alikuwa asili ya nywere nyingi sana (na ndiyo asili tuliyonayo ukoo wetu hadi leo), Sasa alipokuwa katika kuvuna ulezi alikuwa akiweka ulezi kwenye nywere zake na akirudi sehemu ya kulala au geto alikuwa anaukung'uta kwenye chombo ulezi kutoka kwenye nywere zake kwa kitendo hicho alihifadhi ulezi mwingi na kupata mbegu ya kutosha akatoroka na kuelekea milima ya uwanji akaanza kulima ulezi na baadaye alipofanikiwa katika kilimo chake alianza kuleta wabena baadhi kama wafanya kazi katika mashamba yake na waliohamia huko kwa sababu walikuwa katika maeneo ya wawanji nao wakawa wawanji na ndio maana baadhi ya majina ya wabena yapouwanji na ni ndugu zetu sisi kama wakina msigwa, nsemwa au msemwa na wengine wengi,

Katika historia hiyo inagusa Hadi kipindi cha mkwawa kwamba Kuna baadhi ya watoto wa NGUVILA au wajukuu walikuwa ni wanajeshi wa mkwawa kwani walikuwa wakichukuliwa mara kadhaa kwenda kumsaidia mkwawa katika vita zake na wazungu, ndio maana ukienda nhungu Kuna historia ya Moja ya babu zetu kinanguvila alikuwa mahili sana wa kuchezea mikuki na mishale na pia aliwahi kumuua nadhani ni ndugu yake au adui wa ndugu yake kwa kutumia utaalamu huo,

Pia Moja ya kinanguvila alipokea wamissionary wa kilutherani na ndiye mjenzi wa kwanza wa kanisa la KKKT lililoko pale Nhungu,

Najivunia pia kuwa hata Sasa pia dayosisi ya kule askofu wao ni NGUVILA,


Nimefurahi kushiriki kwa sehemu ninachokijua kuhusu sehemu ndogo ya wawanji. EDICKO STANLEY (majadiliano) 15:23, 23 Oktoba 2024 (UTC)Reply

Rudi kwenye ukurasa wa " Wawanji ".