Wawanji ni kabila kutoka wilaya ya Makete, katika milima ya Kipengere ya Mkoa wa Njombe, sehemu ya kusini ya nchi Tanzania. Asilimia kubwa ya Wawanji wapo sehemu za Ikuwo na Matamba, maarufu kama bonde la Uwanji.

Mwaka 2003 idadi ya Wawanji ilikadiriwa kuwa 28,000[1]. Lugha yao ni Kiwanji yenye misamiati ambukizi toka makabila jirani.

Wawanji ni majirani kabisa wa kabila la Wakinga, wakipakanishwa na hifadhi ya Kitulo.

Historia ya Wawanji

hariri

Inasemekana Wawanji walitokea Afrika Kusini, katika lile kundi kubwa la raia waliomkimbia chifu Chakazulu aliyekuwa mkali sana; kundi hilo lilipoingia Tanganyika likagawanyika na kuzaa makabila kama Wangoni, Wapangwa, Wamanda, Wakinga, Wawanji, Wamagoma,n.k

Pia kabila la Wawanji linakuwa na majina ya ukoo yanayofanana na makabila mengine kama Wagogo, hii ni kwa sababu ya muingiliano wa biashara ya kubadilishana vitu iliyokuwepo zamani; wakati huo chumvi ilikuwa bidhaa adhimu sana, kinachoonekana ni kwamba kuna baadhi ya Wawanji walilowea huko kwenye himaya za makabila mengine.

Wawanji ni watu wakarimu sana na kupokea wageni wa aina yoyote bila ubaguzi. Uthibitisho wa hili ni pale wanapoonekana kuishi vyema na makabila yaliyowazunguka kama Wakinga, Wabena, Wanyakyusa, Wasafwa na wengine; pia wanaweza kuoana na makabila yote Tanzania bila kipingamizi.

Makabila jirani huamini kuwa huwezi kufika nyumbani kwa Mwanji ukaondoka bila chakula na pia kama ukienda na chakula chako basi, mtakila wote na wewe utakula chakula chao.

Mazao maarufu yanayostawishwa katika bonde hili ni kama: mahindi, ngano, maharagwe, njegere, viazi mviringo, na kwa kiasi kidogo mtama na ulezi. Lakini pia kuna pareto kama zao la biashara.

Pia Wawanji wana ngoma yao ya asili maarufu kwa jina la Ngadule, ambayo enzi za zamani ilichezwa sana kwenye sherehe mbalimbali na mavuno.

Idadi kubwa ya Wawanji ni Wakristo, wanamwamini Yesu Kristo. Pia Waislamu wapo, lakini si kwa idadi kubwa: kila watu 10 Mwislamu ni mmoja au hakuna kabisa. Hii inajidhihirisha wazi kutokana na kuwepo kwa makanisa mengi kuliko misikiti, mfano mji wa Matamba una msikiti mmoja ambao unafanana na nyumba ya mtu ya kuishi eneo la Mahanji, lakini makanisa yapo kila kitongoji.

Hata hivyo ushirikina una mizizi mirefu bado.

Tanbihi

hariri
  1. Vwanji. A language of Tanzania.
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wawanji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.