https://us.docworkspace.com/d/sIN2I3Pct7dfWhQY

KILIMO CHA NYANYA UKIRIGURU MWANZA

hariri

https://us.docworkspace.com/d/sIN2I3Pct7dfWhQY ALFRED MTENGWA (majadiliano) 03:25, 2 Juni 2021 (UTC)Reply

karibuni 197.186.4.54 10:16, 15 Januari 2024 (UTC)Reply
KILIMO BORA CHA NYANYA UKIRIGURU MWANZA
MWONGOZO BORA WA NYANYA KWA MAVUNO MENGI
NAME : ALFRED MTENGWA
Agronomist Alfred Mtengwa- +255-759-8726-55
UTANGULIZI
KILIMO CHA NYANYA
Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya nizao la kwanza katika mazao ya mboga linalo limwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha namboga  zingine. Na  kwa  mujibu wa  tafiti  mbalimbali zao  la  nyanya ndio  zao  namba mojalinaloweza  kutoa  pesa nyingi  ukilinganisha  na mazao  mengine  ya mbogamboga.  Nyanyahutumika karibu Katika kila mlo. Nyanya ni jamii ya mazao ya Solanaceae, mazao menginemarufu katika kundi hili ni pilipili hoho, biringanya, ngogwe na viazi mviringo. Uzalishaji wanyanya unahitaji uangalizi na matunzo ya hali ya juu katika huduma ya pembejeo. Pamoja nahayo zao hili linaweza kumpatia mkulima faida kutokana na mahitaji yake katika matumizi yakila siku kwenye familia za aina zote.
Hali ya hewa
Nyanya hustawi vizuri kwenye hali ya hewa yenye joto la wastani kati ya nyuzi joto 21 na 32
C na katika mwinuko wa mita 300-1400 juu ya usawa wa bahari na huhitaji maji mengi kiasicha mm 1800 kwa msimu.
Udongo
Udongo tifutifu  wenye  rutuba ya  kutosha  usiotuamisha maji  hufaa  zaidi kwa  kilimo  chanyanya, japo kuna uwezekano wa nyanya kuzalishwa hata katika udongo wenye kichanga aumfinyanzi. Kiwango cha tindikali na chachu katika udongo ( Soil pH) kinapaswa kudhibitiwa.Nyanya hustawi vizuri kwenye pH ya kati ya 5.5 – 75 lakini hustawi vizuri zaidi kwenye pHya 6-6.5 (Soil pH)
Aina za nyanya
Kuna aina kuu mbili za nyanya
Nyanya zinazokuwa ndefu (Indeterminate)
Aina hii ya nyanya huendelea kukua na kuzaa kwa muda mrefu. Hutolewa machipukizi aumaotea  na kubaki  shina  moja au  matawi  mawili tu.  Husegekwa kwa  kutumia miti  mirefu,kamba ndefu na wakati mwingine nyaya hutumika.Nyanya aina hii na mahususi kwa kilimokatika mabanda (greenhouse). Mkulima anaweza kulima aina hii ya nyanya nje lakini anahitajikuwa na nguvu kazi kubwa kwa ajili ya kuweka miti. Ukiilima ndani unaweza vuna kwa mudausiopungua miezi  9  na iwapo  utailima  nje unaweza  vuna  kwa muda  usiopungua  miezi 6mfululizo.Mfano wa mbegu hii ni ; Anna F1, Tylka F1, Eva F1, Uwezo, Moyo, nk.
Nyanya ndefu katika banda ( green house)Nyanya fupi ( Determinate)
Hizi ni nyanya fupi, zinakuwa na kikomo cha kukua ndani ya muda mfupi. Huvunwa kwa muda
mfupi, kiasi  cha  miezi 2-4  tu.Ni  nyanya zinazoshauriwa  kulimwa  kibiashara na  wakulimawenye mashamba makubwa.  Aina hii ya nyanya aipogolewei machipukizi na huwekewa mitimifupi ya kiasi cha mita 1.5-2. Mfano wa aina hii ya mbegu ni Kilele F1, Asila F1, Edeni F1,Nuru F1, Monica F1, Jara F1, Tanya, Mwanga, Riogrand, Imara nk. Mbegu hizi hupatikanakwenye makampuni mbalimbali mfano Mosanto, Rijz zwaan, Balton, syngenta, Royal seeds,kibo seed, East Africa na wengineo wana mbegu aina mbalimbali na nzuri.
NB: Aina hizo mbili za nyanya pia zimegawanyika; kuna mbegu chotara (Hybrid) na mbeguzilizoboreshwa (OPV) na mbegu chotora ndio mbegu nzuri zaidi.
Mfano wa mbegu chotara (Hybrid) ni;
Asila f1, Anna F1, Kilele F1, Edeni F1, Nuru F1, Rambo F1, Monica F1, Milele F1, Jara F1,Tylka F1, Kipato F1, Shanty F1, Imara, nk
Mfano wa mbegu za kawaida zilizoboreshwa ni;Tanya, Rio Grande, Onyx, Tengeru 97, Mwanga, nk
Mahitaji ya mbegu.
Ni  muhimu  kutumia mbegu  bora  kila wakati.  Kiasi  cha gramu  50-100  ya mbegu  hutoshakupanda ekari moja kutegemea njia usiaji, uotaji na nafasi ya kupanda. Mbegu ya nyanya huotabaada ya siku 4-8.
Nyanya Fupi,  nanenane,  2014- Morogoro  Tz.  Ilisimamiwa na  Agronomist  Peter akiwa
Syngenta wakati huo.
Kusia/vitaru.
Kuna aina mbili kuu ya vitaru, vitaru sinia ( Tray) na vitaru vya chini. Vitaru sinia ni vizurisana kwani husaidia kuepuk magonjwa ya ardhini na ukitunzia miche kwenye vitaru sinia michehukua vizuri na kwa haraka zaidi.
Vitaru vya chini pia vimegawanyika, kuna vitaru mbinuko na vitaru mbonyeo. Vitaru mbinukoni vizuri kwani husaidia hewa kuzunguka kwa urahisi.
Kwa kawida miche nyanya huwa tayari kupandikizwa shamba kubwa baada ya siku 21 tangiakumwaga mbegu chini/kusia.
Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa kina cha sentimita 30-45 na kisha andaa matuta yenye upana wa sentimita
150  kutoka  katikati ya  tuta  moja na  lingine.Unaweza  lima bila  matuta  lakini zipo  faidazitokanazo na matumizi ya matuta katika kilimo, baadhi ya faida hizo ni kuwa matuta huwezakuruhusu mizizi kusambaa vema na kupata virutubisho, unyevu na hewa. Matuta pia huondoamaji mengi yaliyozidi shambani hasa wakati wa mvua nyingi.
Upandaji.
Nyanya hupandwa kwa umbali wa nafasi ya sentimita 30 mche na mche na sentimita 60 mstarina mstari ( kwa mbegu za kawaida zilizoboreshwa). Kwa mbegu chotara inshauriwa mche namche iwe sentimita 60 na mstari na mstari iwe sentimita 90.
Panda kwa kutumia mbolea kianzio (starter solution), tengeneza mwenyewe hiyo mbolea kwakutumi DAP ( Chukua 3 Kg za DAP na weka kwenye maji lita 200, hii ndio ratio, hakikishawakati wa kuweka stater haigushi majani ya miche)
Uwekaji miti /usegekaji
Nyanya ni mimea nyenye shina laini lisiloweza kusimama wima bila usaidizi, hivyo basi ilikuweza kuongeza  uzalishaji  kwa kuepuka  magonjwa  ni muhimu  mimea  ya nyanya  iwezekuwekewa  miti ili  isimame  imara bila  kutambaa  ardhini. Zipo  aina  nyingi za  uwekaji  mitikutegemea na aina ya nyanya, kama ni fupi au ndefu na pia hutegemea na upatikanaji wa vifaakama vile miti/fito, waya, nk.
Uwekaji miti hupunguza mashambuzi ya magonjwa na wadudu kwa kuruhusu mzunguko wahewa kupita vema na kuongeza ukuaji mzuri kwa kuruhusu mwanga kupenya kwa urahisi. kwaekari moja inahitaji miti 1800 urefu ni mita 1.5 – 2 na kamba mita 15000 ambayo itakuwezeshakufunga  mizunguko mitatu  weka  mita kwa  muda  muafaka kabla  ya  kupanda au  baada  yakupanda na isizidi siku 14 na mti na mti weka cm 150 usipungue hapo watu wengi hukoseahapa  wanaweka sm  200  au  300  na mimea  ina  anguka kwa  hiyo  maana ya  kufunga  kambainakuwa haipo.
Kupunguza machipukizi/ Maotea na majani
Ni muhimu kwa nyanya ndefu kuondoa machipukizi na kabakia shina moja au mawili tu ilikupunguza msongamano na hivyo mimea huzaa matunda yenye ubora wa kutosha. Kwa nyanyafupi  hakuna   sababu   ya  kupunguzia   lakini   majani  hupunguzwa   matunda   yanapokaribiakokomaa.
Palizi
Magugu hushindana  na  mazao katika  kugombea  virutubisho, mwanga,  hewa  na unyevu.Magugu ni moja ya visumbufu kwa mazao yetu. Shamba lililojaa magugu huvutia wadudu navimelea vya magonjwa  kuweza  kujificha na  kufanya  mashambulizi kwa  mazao  hivyo shartyaondolewe  na  kuacha shamba  likiwa  katika hali  ya  usafi kila  wakati.  Zipo njia  kadhaa  zaudhibiti wa magugu shambani, kama palizi, kung’oa kwa mkono, kutumia viuagugu kabla nabaada ya kupanda, kabla ya kupanda kama shamba lina majani unashauriwa kutumia viuaguguvinavyoua magugu yote mfano wa viuagugu hivo ni ;
➢ Kalach 480 SL (Glyphosate 360 g/ℓ (480 g/ℓ as IPA salt), Kipimo: 1 - 6 ℓ/ha (or 80 -
480 mℓ kwa bomba 20 L kulingana na aina ya magugu na ukubwa wa magugu. Puliziawakati  magugu  yapo  kwenye  hali ya  ukuaji,  yasiwe yameanza  kukauka  na kamamagugu ni makubwa tumi kipimo kikubwa kinachoshauriwa.
➢ Volsate 360 SL (Glyphosate 360 g/ℓ (480 g/ℓ as IPA salt) Kipimo: 1 - 3 ℓ/ha (or 80 -
240 mℓ kwa bomba  20 L
NB: Usitumie viuagugu hivi kama tayari umeshapanda, vitaua mimea yako.Viuagugu ambavyo huweza kuua magugu na nyanya zikabaki ni:
Pantera 40 EC (Quizalofop-P-Tefuryl 40 g/ℓ): Kipimo: 1 – 3 ℓ /ha (au 80 - 320 mℓ
per 20 L, tumia kipimo kikubwa kama magugu/majani ni makubwa.
Centurion 120 EC  (Clethodim 120 g/ℓ): Kipimo: 1 – 2 ℓ/ha (au 80 - 160 mℓ kwa
bomba 20 L
NB: Viuagugu hivi huua magugu aina ya nyasi tu, kama kuna magugu/majani yenye majanimapana hayatakufa na hivyo unashauriwa kukagua shamba lako kuangalia aina ya magugu nakama mengi ni nyasi ndio utumie hivi viuagugu tofauti na hapo usitumie.
Mbolea.
Nyanya kama yalivyo mazao mengine huhitaji rutuba ya kutosha yenye virutubisho mbalimbalikama vile  naitrojeni,  fosforasi, potasium,  manganizi,  kalshamu n.k.   Virutubisho  hivyovinahitajika kwa kiwango na wakati tofauti na hufanya kazi tofauti kwa mmea, kwa hiyo nimuhimu kuweka mbolea zenye virutubisho vyote na kwa wakati muafaka ili kupata mazao bora.
Unapopanda nyanya anza na starter iliyotengenezwa kutoka kwenye DAP, kutengeneza hiyostarter changanya 3 kg ya DAP kwenye maji lita 200 na kisho weka 250 ml kwa kila shina,hakikisha maji ya mbolea hiyo hayagusi majani.
Baada ya hapo, subili siku 5-7 na weka DAP au Yara otesha au NPK,   kiasi cha 5g kwa kilashina na baada ya siku 21 tangia uweke DAP weka Yalamira winner/NKP kiasi cha 5g kwashina, baada ya siku 14-21 tangia uweke yalamila winner weka Yalavita nitrabo au CAN kiasicha 5 – 10g kwa kila shina. Baada ya kuweka mbolea hizi subili siku 21 na weka MOP kiasicha 5 -10 g kwa kila shina na endelea kuweka CAN, NPK NA MOP kwa kubadili kila baadaya siku 21 hadi mwisho wa mavuno.
Madini ya Naitrogen(N)
Ni madini muhimu kwa ajili ya ukuaji, hasa utengenezaji wa majani ya rangi ya kijani kibichi.Madini haya huhitajika sana wiki chache baada ya kupandikiza. Rangi ya kijani ni muhimu kwaajili ya utengenezaji wa chakula cha mimea. Kunapokuwa na upungufu wa naitrogeni, rangi yamajani hupauka kuwa njano na mimea hudumaa. Hata hivyo, haifai kutumia naitrojeni nyingikupita kwani ikizidi, mimiea huwa na majani mengi bila matunda na hivyo kuathiri mavunoPanapokuwa na upungufu wa naitrojeni, inashauriwa kutumia mbolea za chumvi kama CAN,UREA, SA na NPK.
Dalili za upungufu wa naitrojeni, majani kuwa njano
Fosforasi (P)
Ni madini muhimu kwa utengenezaji wa mizizi na matunda kwa mimea na huhitajika maramoja wakati wa kupanda. Inapatikana katika mbolea aina ya Minjingu, DAP, TSPLol NPK n.k.Madini haya pia haipaswi kutumika kwa wingi kupita kiasi kwani ikitumika kupita kiasi huzuiamimea  kuchukua kutoka  ardhini  madini joto  aina  ya zinki.  Ili  kutambua upungufu  wakirutubisho cha fosforasi katika mimea, rangi ya majani na shina hubadilika na kuwa rangi yazambarawe hasa sehemu za pembeni, ncha huonekana kama zimeungua na yale majani ya chinihubadilika na kuwa ya kahawia na mwisho hudondoka.
Upungufu wa fosforasi, majani na shina huwa zambarawe
Madini aina ya Potashi(K)Ni muhimu wakati wa maua, matunda kwa mmea na kuimarisha ubora wa mbegu. Madini yapotash pia  huimarisha  kinga ya  mimea  dhidi ya  mashambulizi  ya magonjwa  mbalimbali .Upungufu  wa  madiniya potash  huambatana  na dalili  kama  vile  majani kuonekana  kamayamebabuka kwa moto sehemu za pembeni na majani kuwa ya njano katikati ya mishipa yakena pembeni. Dalili hizi huanza katika majani ya chini ya mmea na kupanda juu. Dalili katkamatunda yanapoiva ni kupauka na kutokuwa na rangi nyekundu iliyokolea.
Dalili za upungufu wa potash katika majani na katika tunda.Madini ya Magnesiam (Mg)
Ni madini muhimu katika kuhakikisha ubora wa matunda . Dalili za upungufu wa madini hayani pamoja  na  majani kuwa na  unene  na uzito  kupita  kiasi. Dalili  nyingine  za upungufu  wamagnesiam ni mishipa katika majani hupoteza rangi asilia ya kijani iliyokolea na kuwa na rangiiliyopauka. Upungufu hutokea hasa katika udongo wenye kichanga na tindikali nyingi na piakatika udongo wenye maji kupita kiasi na katika hali ya ukame mkali.Panakuwa na upungufuwa madini haya, inashuriwa kutumia mbolea zenye madini haya kama magnesium sulphate.
Dalili za upungufu wa magnesiam katika majani.Madini chokaa ya kalisi (Ca)
Nyanya  ni  zao linalohitaji  sana  madini haya.  Endapo  madini haya  yatapungua,  vitako vyamatunda  ya  nyanya hubadilika  rangi  na kuwa  nyeusi  na kisha  husinyaa  na kuoza.  Ainambalimbali  za nyanya  pia  hutofautiana katika  mahitaji  ya madini  haya  kwani zipo  ainazinahitajika kwa wingi sana na hizo huathirika zaidi panapokuwa na upungufu. Inashauriwakutumia mbolea aina ya calcium nitrate na kusambaza chokaa shambani ili kuinua kiwango chamadini haya panapokuwa na upungufu. Pia mwagilia kwa wakati, calcium husafiri kupitia njiaya maji na hivyo panapokuwa na umwagiliaji usiokua na mpangilio huathili pia upatikanaji wacalcium, pia hakikisha ardhi yako imelimwa vizuri kuhakikisha mizizi inapenya vizuri ardhini.
Dalili za upungufu wa chokaa (calcium)
Angalizo: Kabla  ya  kutumia aina  yoyote  ya mbolea,  ni  vema kupata  ushauri  wa kitaalamukuhusu  aina,  kiasi, namna  na  wakati wa kutumia.  Inapobidi  ni vema  kupima  udongo kujuavirutubisho vilivyopo na kiasi chake pamoja na tindikali (Soil pH) na kiwango cha chumvi (EC)katika udongo.
Umwagiliaji
Nyanya ni zao linalohitaji maji mengi hasa wakati wa kupandikiza, wakati wa kutoa maua nawakati wa kutoa matunda. Ni muhimu pia kuwa na uwianao mzuri wa umwagiliaji muda wotebadala ya umwagiliaji usiotabirika. Kunapokuwa na maji kidogo wakati wa matunda, matatizokama upungufu wa madini ya kalisi hujitokeza sana hata kama katika udongo hakuna upungufuwa  madini hayo.  Hii  inatokana na  ukweli  kwamba madini  ya  kalisi huhitaji  maji  mengi ilikuyeyuka na kuweza kufyonzwa na mimea. Dalili za upungufu wa maji hupelekea upungufuwa madini ya kalisi na katika nyanya matunda kuoza katika kitako na kuwa na rangi nyeusi.Kuna umwagiliaji wa matone, mifereji, n.k.
Matandazo
Matandazo ya masalia ya mpunga, mahindi, mtama, migomba pamoja na nyasi kavu hutumikakufunika udongo  shambani  ili kupunguza  upotevu  wa unyevu.  Matandazo  husaidia piakudhibiti magugu na pindi yanapoozo huongeza rutuba ya udongo (mboji). Matandazo huwekauwiano mzuri wa joto la udongo la udongo na huwa chachu ya kuzaliana kwa wadudu muhimu(fauna na flora) katika kuboresha uhai wa udongo kama vile minyoo ardhi n.k.
Muzunguko wa Mazao
Kilimo cha mzunguko wa mazao ni muhimu kuzingatiwa wakati wote kwani husaidia kudhibitimaambukizi ya wadudu na magonjwa kwa mazao. Mzunguka wa mazao pia hutoa fursa kwamatumizi sahihi  ya  ardhi na  udongo  kutokana na  ukweli  kuwa mazao  hutofautiana  katikamahitaji  na matumizi  ya  madini ardhini  bali  pia yapo  mazao  ambayo husaidia  katikakurutubisha udongo. Hivyo inashauriwa kubadili nyanya na jamii yake kila baada ya msimu.Mazao ya jamii ya nyanya ni kama vile, pilipili, biringanya, ngogwe, viazi mviringo n.k. Ilikuwa na mzunguko bora wa mazao katika shamba la nyanya waweza kulima kwa kubadilishana kabichi, vitunguu, maharage, karoti n.k.
Wadudu
Nzi weupe (Whitefly)
Ni wadudu waupe wadogowadogo wanao fanana na nzi na huruka unapotikisa mmea. Waduduhawa hushambulia  kwa  kufyonza majimaji  ya  majani, hasa  majani  machanga. Mbali  nakufyonza majimaji ya mimea huambukiza magonjwa ya virusi ambayo ni hatari na hayana tiba.
Nzi weupe
Udhibiti
Tumia viuatilifu vinavyoshauriwa na wataalamu. Usafi wa shamba na uondoaji wa masalia yamazao na kuyachoma mara moja baada ya mavuno hupunguza kuzaliana kwa wadudu hawa nahivyo kupunguza mashambulizi.
Viuadudu ambavyo hufanya vizuri kudhibiti wadudu hawa ni:
Evisect 50 SP (Thiocyclam 50 %): Kipimo: 500 – 750 g/ha (or 25 g / 20 L. Hii ndiokiuadudu bingwa No.1 kwa hawa wadudu, unapopulizia hakikisha kila jani linashikakiuadudu na rudia kupulizia kila baada ya siku 7 – 14 kama wadudu bado wapo, kaguamimea yako kabla ya kupulizia.
Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/ℓ + Lambdacyhalothrin 60 g/ℓ + Acetamiprid 32g/ℓ): Kipimo: 250 mℓ/ha au 20 mℓ / 20 ℓ.
Uniron 100 EC (Novaluron 100 g/ℓ): Kipimo: 350 mℓ/ha (au 20 mℓ / 20L
Thiamex 250 WG (Thiametoxam 250 g/kg): Kipimo: 600-800 g/ha (or 12-16 g /20 ℓ
Utitiri mwekundu (Redspider mites)
Hawa  ni  wadudu wadogo  wenye  rangi nyekundu.  Hujilinda  kwa utando  kama  buibuiwafanyavyo. Hawa hufanya uharibifu kwa kula majani hivyo majani huwa na madoa madoamadogo  yenye rangi  ya  njano. Wadudu  hawa pia  hula matunda  na  kusababisha michubukomidogo midogo yenye rangi ya njano au nyeupe iliyofifia.
Utitiri mwekundu/ yebo yebo ( Red spinder mites)Udhibiti
Tumia viuatilifu kwa kufuata maelekezo ya wataalamu, Usafi wa shamba na mazingira yakehasa kwa kuondoa magugu ya jamii ya nyanya kama vile ndulele na mnafu karibu na shambahupunguza  mazalia. Matumiza  ya  makingo hai  pia  hunguza mashambulizi  kutoka  katikamashamba ya jirani. Wadudu hawa huathiri sana wakati wa kiangazi na pia hupendelea sanandani ya banda (green house)
Baadhi ya viuatilifu vinavyodhibiti wadudu hawa ni:
ABALONE 18 EC (Abamectin 18g/l): Kipimo: 250- 500 mℓ/ha au 10 - 20 mℓ / 20 ℓ.
Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250 mℓ/haau  20 mℓ / 20 ℓ.
FLORAMITE® 240 SC (bifenazate 240 g/L): Kipimo: 10 mℓ/20 L
Wadudu mafuta/kimamba (Aphids)
Hawa ni wadudu wanaofyonza majimaji kwenye majani. Wana rangi  mbalimbali kama vilenyeusi,  kijani, njano,  n.k.  na huwa  mbawa.  Kama walivyo  nzi  weupe, wadudu  mafuta  piahusambaza magonjwa ya virusi na pia husababisha unato unaosababisha  ugonjwa wa masizi(soot mold) ambao hutanda na kuweka rangi nyeusi kwenye majani ya mimea, matunda na hatamatawi.
Wadudu mafuta kwenye majani ya nyanya.
Udhibiti
Tumia viuatilifu kwa kufata maelekezo ya wataalam.
Viuadudu ambavyo hudhibiti vizuri hawa wadudu ni:
Attakan C 344 SE (Imidacloprid 200 g/ℓ + Cypermethrin 144 g/ℓ): Kipimo: 250 mℓ
/ha (au 20 mℓ / 20 L -Huyo ndio bingwa No. 1
Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/ℓ + Lambdacyhalothrin 60 g/ℓ + Acetamiprid 32
g/ℓ): Kipimo: 250 mℓ/ha au 20 mℓ / 20 ℓ.
Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250
mℓ/ha au  20 mℓ / 20 ℓ.
Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/ℓ + Acetamiprid 16 g/ℓ): Kipimo: 1ℓ/ha au 20 – 40
mℓ
Funza wakataji (Cutworms)
Funza  hawa  ni wafupi  na  wanene hukaa  ardhini.  Wanaposhikwa na  kuwekwa  kiganjani,hujikunja na kuwa mviringo. Wakati wa mchana hujificha ardhini na huibuka wakati wa usikuna kukata mimea michanga hasa wakati wa kupandikiza Mashambulizi makubwa huonekanakatika mashamba yenye magugu, yenye mboji nyingi na hasa wakati wa mvua. Funza hawahushambulia nyanya kabla ya kuanza kutoa matunda.
Funza wakataji ( Cutworms)
Udhibiti
Tumia viuatilifu kwa maelekezo ya wataalamu.
Baadhi ya viuatilifu vinavyofanya vizuri kuua hawa wadudu ni:
Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/ℓ + Lambdacyhalothrin 60 g/ℓ + Acetamiprid 32g/ℓ): Kipimo: 250 mℓ/ha au 20 mℓ / 20 ℓ.
Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250
mℓ/ha au  20 mℓ / 20 ℓ.
Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/ℓ + Acetamiprid 16 g/ℓ): Kipimo: 1ℓ/ha au 20 – 40
mℓ
NB: Pulizia wakati wa jioni sana au usiku kabisa kama inawezekana.
Funza wa vitumba (American Bollworm)
Hawa  pia  hushambulia nyanya  mara  tu matunda  yanapoanza.  Hutoboa na  kuingia  katikamatunda yanapokuwa madogo. Ni rahisi kuwadhibiti funza hawa wanapokuwa wadodgo lakinipindi  wakiwa wakubwa  ni  vigumu kuwadhibiti  na  wakati huo  pia  huwa wameshakwishakusababisha hasara kwa kutoboa matunda na kuyaozesha.
Funza wa vitumba ( American Bollworm)
Viuadudu ambavyo hudhibiti wadudu hawa ni;
Attakan C 344 SE (Imidacloprid 200 g/ℓ + Cypermethrin 144 g/ℓ): Kipimo: 250 mℓ
/ha (au 20 mℓ / 20 L -Huyo ndio bingwa No. 1
Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/ℓ + Lambdacyhalothrin 60 g/ℓ + Acetamiprid 32
g/ℓ): Kipimo: 250 mℓ/ha au 20 mℓ / 20 ℓ.
Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250
mℓ/ha au  20 mℓ / 20 ℓ.
Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/ℓ + Acetamiprid 16 g/ℓ): Kipimo: 1ℓ/ha au 20 – 40
mℓ
Minyoo Fundo (Nematodes)
Ni minyoo wadogo sana ambao huathiri mizizi kwa kuchimba ndani ya mizizi na kusababishavifundo na mizizi kuvimba. Uvimbe na vifundo huathiri uwezo wa mizizi kunyonya maji navirutubisho katika kutoka ardhini, hivyo miea hudhoofika, hunyauka, hudumaa na kushindwakuzaa.
Madhara ya minyoo fundo
Udhibiti
Panda  aina  ya nyanya  zinazo  stahimili (  Resistant  varieties), tumia  mzunguko  wa mazaokupunguza mashambulizi. Pia unaweza kutumi dawa kama Solvigo 108 SC (Thiamethoxam
72g/l  +  Abamectin 36g/l),  Bio-Nematone  1.15%WP (Paecilomyces  Lilacinus  1.15%), RealTrichoderma  (Real  Trichoderma), Furaban  3GR  (Carbofuran 3g/kg),  NEMACUR  5 GR(Fenamiphos), PL-Plus (Paecilomyces lilacinus Spores 2 x 109)
Chorachora ( Leaf Miners)
Mabuu  ya  wadudu hawa  hula  majani ya  nyanya  na kutengeneza  michirizi  kama ramani.Michilizi hii pia huonekana kama machimbo ya mgodi na ndiyo chimbuko la jina la waduduhawa  kwa  kiingereza. Michirizi  hii  hupunguza maji  katika  majani na  hivyo  kusababishakudondoka, hupunguza uwezo wa mimea kutengeze chakula chake na kupunguza mavuno
Chorachora ( Leafminer)
Baadhi ya viuatilifu vinavyodhibiti wadudu hawa ni:
ABALONE 18 EC (Abamectin 18g/l): Kipimo: 250- 500 mℓ/ha au 10 - 20 mℓ / 20 ℓ.
Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250 mℓ/haau  20 mℓ / 20 ℓ.
FLORAMITE® 240 SC (bifenazate 240 g/L): Kipimo: 10 mℓ/20 L
Kanitangaze (Tuta absoluta)
Huyu  ni  mdudu mpya,  kwa  mara kwanza  aliripotiwa  Tanzania mwaka  2014.  Mdudu huyuhuweza kula majani, shina na matunda, kwa hiyo huweza kusababisha hasara asilimia 100.Huyu mdudu ni sugu kwa viuadudu vingi, kuna viuadudu maalumu kwa huyu mdudu na hivyoviuatilifu iwapo  utapulizia  aina moja  mfulilizo  kwa muda  mrefu,basi  kanitangaze huwezakujenga usugu wa viuadudu husika. Kwa hiyo inashauriwa kupulizia kiuadudu kwa kubadili ilikuepuka usugu  wa  viuatilifu. Mdudu  huyu  ana hatua  nne  za ukuaji  amabazo  ni; Yai,funza/kiwavi, bundo/pupa na kipepeo. Hatua ambayo ni mbaya sana ni ya funza/kiwavi kwanifunza ndio huaribu mimea.
Viuadudu ambavyo hudhibiti wadudu hawa ni;
Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250
mℓ/ha au  20 mℓ / 20 ℓ.
Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/ℓ + Acetamiprid 16 g/ℓ): Kipimo: 1ℓ/ha au 20 – 40
mℓ
Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/ℓ + Lambdacyhalothrin 60 g/ℓ + Acetamiprid 32g/ℓ): Kipimo: 250 mℓ/ha au 20 mℓ / 20 ℓ.
Evisect 50 SP (Thiocyclam 50 %): Kipimo: 500 – 750 g/ha (or 25 g / 20 L. Hii ndio
kiuadudu bingwa No.1 kwa hawa wadudu, unapopulizia hakikisha kila jani linashikakiuadudu na rudia kupulizia kila baada ya siku 7 – 14 kama wadudu bado wapo, kaguamimea yako kabla ya kupulizia.
Uniron 100 EC (Novaluron 100 g/ℓ): Kipimo: 350 mℓ/ha (au 20 mℓ / 20L
NB: Chagua viuadudu 3 na pulizia kwa kubadili.
MAGONJWA
Bakajani wahi (Early Blight)
Ni ugonjwa wa fangasi ukungu unaoshambulia mimea ya nyanya kwa kiasi kikubwa. Ugonjwahuu hushambulia zaidi katika kipindi cha mvua . Dalili za ugonjwa huu ni kuwa   na madoamadogo madogo yenye rangi nyeusi au rangi ya kahawia kwenye majani hasa ya chini, matundana shina. Miche midogo kwenye kitalu inaposhambuliwa hunyauka na kufa, na miche mikubwahudondosha majani na matunda na kunyauka kwa shina na hatimaye kufa.
Mashambulizi ya bakajani wahi (Early blight)
Udhibiti
Hakikisha usafi wa shamba na ng’oa masalia ya mazao na kuchoma moto mara moja baada yakuvuna.Zingatia kilimo  cha  mzunguko wa  mazao.  Tumia viuatilifu  sahihi  kwa kufuatamaelekezo ya wataalam.
Baadhi ya viuakuvu venye uwezo wa kudhibiti ugonjwa huuEvito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/ℓ + Tebuconazole 277 g/ℓ): Kipimo: 400 – 600
mℓ/ha (au 16 – 24 mℓ /20 L
Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 - 2.00kg/ha (au 60 to 80 g /20
Banko 720 SC (Chlorothalonil 720 g/ℓ): Kipimo: 1.4 - 2.1 ℓ /ha (au 50 - 80 mℓ / 20 L
Banko 500 SC (Chlorothalonil 500 g/ℓ): Kipimo: 2 - 3 ℓ /ha (au 60 - 100 mℓ / 20 L
Cuprocaffaro 50 WP (Copper oxychlorid 500 g/kg):  Kipimo: 2.7 - 3 kg /ha (au 50 -
100 mℓ / 20 L
INNOVEX 360EC, Cyproconazole
Bakajani chelewa (Late blight)
Ni ugonjwa hatari sana hasa katika kipindi cha mvua na baridi ya wastani. Dalili za ugonjwahuu ni  kuwa na  mabaka makubwa  yenye  majimaji kwenye  matunda,  shina na  hata  majani.Mabaka yenye majimaji hutokea hasa sehemu ya juu ya matunda. Mimea inaposhambuliwa naugonjwa huu hufa katika kipindi kifupi.
Madhara ya bakajani chelewa ( late blight)
Udhibiti
Zingatia kilimo  cha  mzunguko wa mazao.  Zingatia  kanuni za  kilimo  bora kama kupogoleamajani, kusega na kutumia matandazo. Ondoa masalia ya mazao shambani mara moja baada yamavuno kupunguza  vimelea  shambani. Tumia  viuatilifu  sahihi kwa  kufuata  maelekezo yawataalum.
Baadhi ya viuakuvu venye uwezo wa kudhibiti ugonjwa huu ni
Evito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/ℓ + Tebuconazole 277 g/ℓ): Kipimo: 400 – 600
mℓ/ha (au 16 – 24 mℓ /20 L
Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 - 2.00kg/ha (au 60 to 80 g /20
Banko 720 SC (Chlorothalonil 720 g/ℓ): Kipimo: 1.4 - 2.1 ℓ /ha (au 50 - 80 mℓ / 20 L
Banko 500 SC (Chlorothalonil 500 g/ℓ): Kipimo: 2 - 3 ℓ /ha (au 60 - 100 mℓ / 20 L
Cuprocaffaro 50 WP (Copper oxychlorid 500 g/kg):  Kipimo: 2.7 - 3 kg /ha (au 50 -
100 mℓ / 20 L
Ivory 72W.
Madoadoa na mnyauko bacteria.
Mnyauko bacteria  ni  ugonjwa hatari  unaosababishwa  na bakteria  jamii  ya  Pseudomonassolanacearum ambao husababisha mnyauko na kufa kwa mimea ghafla. Dalili za maambukiziya ugonjwa huu huonekana mara tu matunda yanapoanza. Bakteria wanaosababisha ugonjwahuu huishi ardhini katika udongo kwa muda mrefu na hushambulia mimea kupitia mizizi, aumajeraha katika mimea wakati wa kuhamisha miche toka kitaluni na kupandikiza. Mazingirabora kwa bakteria hawa kufanya mashambulizi ni hali ya joto na unyevunyevu katika udongo.Vimelea hawa wakishaingia katika mishipa ya mimea huziba njia za mfumo wa mzunguko wamaji katika mimea hivyo mimea hunyauka kwa haraka, bali rangi ya mimea hubakia na rangiya kijani na bila madoa. Dalili hii husaidia kutofautisha ugonjwa huu na ule wa mnyauko fusari.
Dalili nyingine zinazotofautisha huu na mnyauko fusari ni pale unapokata shina katika sehemuya chini  karibu  na udongo,  sehemu  ya katikati  ya  ndani huwa  na  majimaji yenye  rangi  yakahawia na hatimaye kuwa na tundu. Namna nyingine ya kutofautisha mnyauko bakteria namnyauko fusari pamoja na mnyauko vetisilia ni kukata shina na kutumbukiza katika glasi yamaji. Endapo majimaji ya rangi ya maziwa yatatoka, ni udhibitisho wa kuwa ugonjwa husikani  mnyauko bakteria.  Namna  nyingine ya  kutofautisha  magonjwa haya  ni  kuwa, katikamnyauko bakteria, mimea huanza kunyauka kutokea juu wakati mnyauko fusari na mnyaukovetsilia mimea huanza kunyauka chini kwenda juu.
Mnyauko bacteria
Madoadoa yanayosababishwa na bacteria
Udhibiti
Tumia aina ya nyanya zinazohimili na kustahimili mashambulizi, tumia mzunguko wa mazaowa muda mrefu, hasa kwa kuhusisha mazao jamii ya mtama, usipande nyanya katika shambalililopandwa   migomba  msimu   uliotangulia.   Zamisha  maji   shambani.   Hakuna  viuatilifuvinavyofanya vizuri lakini dawa yoyote yenye copper inasaidia kupunguza tatizo hili,
Baadhi ya viuakuvu venye uwezo wa kudhibiti ugonjwa huu ni
Cuprocaffaro 50 WP (Copper oxychlorid 500 g/kg):  Kipimo: 2.7 - 3 kg /ha (au 50 -
100 mℓ / 20 L
Mnyauko Fusari ( Fusarium wilt)
Ni ugonjwa hatarii wa ukungu/fangasi jamii ya Fusarium oxysporum. Dalili za ugonjwa huu nikudumaa, kubadilika rangi na kuwa njano na kahawia na kisha kunyauka. Vimelea wa ugonjwahuu huishi ardhini na hushambulia miea kupitia katika mizizi. Vimelea wakishaingia huzibamishipa ya kupandisha maji (xylem) na hivyo miea husinya na kushindwa kuzaa na hatimayekufa.
Waweza kutambua ugonjwa huu kwa kuchubua shina katika sehemu ya karibu na ardhi kwendajuu na utaona rangi ya shina ikiwa imebadilika na kuwa ya kahawia, sehemu ya juu karibu naganda. Tofauti na mnyauko baktria ambapo sehemu ya katikati ndio hubadilika rangi na ile yanje karibu  na  ganda huwa  nyeupe.  Mashambulizi ya  mnyauko  fusari huenda  kwa  kasiikilinganishwa na yale ya mnyauko vetisilia na hiyo diyo tofauti kubwa ya magonjwa haya.Ugonjwa huu hushamiri zaidi katika mazingira ya joto na udongo wenye tindikali kiasi. Nirahisi kuchanganya kati ya ugonjwa huu na ule wa mnyauko vetisilia kwani hufanana sana.Vimelea wa ugonjwa huu hushamiri sana katika mazingira ya joto na sehemu yenye udongowenye majimaji.
Hakuna kiuatilifu aina yoyote kinachoweza kutibu ugonjwa huu kwa 100% hivyo inashauriwamara baada ya ugonjwa kujitokeza, ng’oa na choma moto mimea yote iliyoathirika na baada yahapo pulizia dawa za ukungu mimea iliyobaki.
Njia nyingine za kudhibiti ni kutumia mzunguko wa mazao kwa kupanda nyanya katika shambahusika mara moja kila baada ya miaka minne. Katika kipindi hicho pia epuka kupanda mazaojamii ya nyanya kama vile ngogwe, pilipili, biringanya, n.k
Ni muhimu pia kudhibiti minyoo fundo kwani hii hudhoofisha mimea na kusababisha vidondana hivyo kurahisisha kujipenyeza kwa vimelea wa mnyauko fusari.
Viuatilifu hivi hapa chini huweza kupunguza tatizo kwa asilimia furani.
Evito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/ℓ + Tebuconazole 277 g/ℓ): Kipimo: 400 – 600
mℓ/ha (au 16 – 24 mℓ /20 L
Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 - 2.00
Ungonjwa wa kata kiuno.
Ni  ugonjwa  unaosababishwa na  vimelea vya ukungu  (fungi)  vilivyo tapakaa  katika  udongosehemu nyingi. Kuwepo kwa msongamano wa mimea na kukosekana kwa mtiririko bora wamaji ardhini  husababisha  mazingira bora  ya  kuenea kwa  mashambulizi  ya ugonjwa  huu.Ugonjwa huu hushambulia zaidi miche vitaluni na dalili zake ni kunyauka ghafla kwa michesentimita chache usawa wa ardhi. Maji yakizidi ugonjwa huu huathiri zaidi.
Kata kiuno ( Damping off)
Udhibiti.
Tumia mbegu ambazo zina chanjo ya mbegu na ni vyema kabla ya kusia hata kam mbegu inadawa ni vizuri kuweka dawa tena. Chanjo nzuri ya mbegu ni Seed plus 30 WS (Imidacloprid
100g/Kg + Metalaxyl 5g/Kg + Carbendazim 5g/kg). kipimo ni 10g za dawa unawekakwenye kilo 4 za mbegu lakini kwa mbegu za mbogamboga unafanya kukadiria tu, hainamadhara hata dawa ikizidi.
Pia mara tu baada ya miche kuota tumia dawa ya ukungu kama vile:
➢ Ivory M 72 WP (Mancozeb 64 % + Metalaxyl 8 %): Kipimo: 50g/20L
➢ Evito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/ℓ + Tebuconazole 277 g/ℓ): Kipimo: 400 – 600
mℓ/ha (au 16 – 24 mℓ /20 L
➢ Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 - 2.00
Ubwiri unga.
Huu pia ni ugonjwa wa ukungu, dalili zake kwenye majiani utaona ungaunga ua rangi kamamajivu.
Ubwiri unga ( Powdery mildew)
Udhibiti.
Eminent Star 312.5 SE (Chlorothalonil 250 g/ℓ + Tetraconazole 62.5 g/ℓ) Kipimo: 2
ℓ/ha (au 80 mℓ20 L
Procure 480 SC (Triflumizole 480 g/ℓ): Kipimo: 500 – 1000 mℓ /ha (au 20 - 40 mℓ /
20 L
Evito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/ℓ + Tebuconazole 277 g/ℓ): Kipimo: 400 – 600
mℓ/ha (au 16 – 24 mℓ /20 L
Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 - 2.00kg/ha (au 60 to 80 g /20
Magonjwa ya virusi
Magonjwa haya huambukizwa kupitia mbegu ama husambazwa na wadudu kama nzi weupe,wadudu mafuta (Vimamba), wanyama ikiwa ni pamoja na binadamu kwa kupitia vifaa vya kazi.Mashambulizi makali huonekana wakati wa joto kali na ukame. Dalili za magonjwa haya nikudumaa na majani kukunjamana yakipinda kuelekea juu, kutoa matawi mengi na majani kuwana rangi ya njano, nyeupe au zambarawe. Moja ya magonjwa ya virusi ni Tomato Mosaic Virus( TMV)
Tomato Mosaic Virus ( TMV)-Ugonjwa wa virusi kwenye nyanya.
Udhibiti
Ondoa  mara  moja mimea  iliyo  shambuliwa na  kuiharibu  ( choma  moto)  mbali na  shamba,zingatia usafi wa shamba, thibiti wadudu waenezao virusi na kusafisha vifaa vya kupogoleakama visu kila unapomaliza kuhudumia mmea mmoja. Epuka kuvuta sigara kwenye shamba lanyanya na dhibiti wadudu hasa nzie weupe.
Matatizo mengine.
Matunda kupasuka
Matunda huweza  kupasuka  yanapokuwa makubwa  karibia  na muda  wa    kukomaa. Ipomipasuko ya mviringo na mingine yenye sura ya nyota.  Mipasuko hii hutokea kutokana nakutokuwa  na umwagiliaji  wenye  mpangilio mzuri,  mara  maji mengi  mara  kidogo. Hali  hiihujitokeza zaidi wakati wa vipindi vya jua kali na mvua vinapofuatana. Tatizo hili husababishahasara kwa mkulima kwani matunda hupoteza thamani na pia majeraha husababisha kuoza nahivyo kupunguza thamani na hatimaye mauzo kidogo.
Kupasuka kwa matunda
Udhibiti.
Kuwa  na  mpangilio mzuri  wa  umwagiliaji. Matumizi  ya  umwagiliaji kwa  mjia  ya matonehuepusha tatizo hili na pia weka mbolea kama inavyoshauriwa
Alfred Mtengwa
alfredhungwi@gmail.com
Kilimo ni sayansi 197.186.4.54 10:19, 15 Januari 2024 (UTC)Reply