HISTORIA YA NYERERE IMEKOSEWA hariri

Ndugu zangu katika wikipedia nimesikitishwa na historia ya hayati mwl.Julius K Nyerere.Sidhani kama aliyeandika amefuatilia vizuri historia ya mwalimu.Elimu ya mwalimu imeandikwa kuwa ni shahada ya kwanza B.A. na ukweli ni kwamba mwalimu alikuwa na shahada ya uzamili ya uchumi na historia.Naomba waandishi tusome vizuri na kufanya utafiti kabla ya kuandika kwa ushauri unaweza kusoma katika links hizi kupata habari za mwalimu: http://en.wikipedia.org/wiki/Julius_Nyerere http://www.infed.org/thinkers/et-nye.htm http://www.zmag.org/sustainers/content/1999-10/tributetonyerere.htm au kama unapenda mijadala na habari zaidi kuhusu shujaa huyu wa Afrika,jiunge kwenye http://groups.yahoo.com/group/nyerereforums/


Karibu kwenye wikipedia ya Kiswahili hariri

Karibu kwenye wikipedia ya Kiswahili! Ujisikie huru kuchangia, kuandika au kusahihisha makala na kushauriana nasi wengine. Tazama Msaada wa kuanzisha makala kabla hujaanza menginevyo andika maswali yako.

Kama unadhani ya kwamba umegundua kosa katika makala basi usahihishe ukiwa na uhakika. Kama ni jambo la mawazo ni vema kuandika kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano wa makala na kusubiri siku. Hii itaongeza maelewano. Kwa hiyo ni vema ukipeleka hoja kwenye ukurasa wa majadiliano wa makala ya "Nyerere" au kusahihisha moja kwa moja. Yaani BA au MA si jambo la mawazo ni swali la ndiyo au hapana kwa hiyo ni rahisi kusahihisha. --Kipala 21:18, 24 Septemba 2007 (UTC)Reply