MWALI IBRAHIM MBANGO, alizaliwa kigoma ujiji katika hospitali ya maweni mkoani humo, Mwali ni mtoto wanne katika familia ya watoto tisa ya Mzee Mbango ambaye ni Afisa elimu wa mkoa wa Manyara.

Katika historia ya elimu aliweza kusoma katika shule mbalimbali ambapo elimu ya msingi alifanikiwa kuipata mwaka 1995 katika shule ya msingi ya Ngarenaro iliyopo mkoani Arusha.

Wkati huo anaanza shule alikuwa tayari anajua kusoma vizuri na hata kufanya maswali ya hesabu mbalimbali kitu ambacho kiliwafurahisha walimu wake kwani aliweza kufanikiwa kushika nafasi za juu katika matokeo yake.


Lakini hakuweza kumalizia elimu yake hapo alihamia mkoani Kigoma na kuendelea katika shule ya msingi Kiezya wakati huo baba yake ni Afisa elimu wa wilaya wa mkoa huo lakini pia hakuweza kusoma sana kwani mzazi wake huyo alipata uhamisho na kuwa Afisa elimu wa mkoa wa Rukwa ambapo alienda kumalizia darasa la saba katika shule ya msingi Chemchem na kufanikiwa kufaulu.

Mwali alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya Kantalamba mwaka 2001 ambapo alisoma hadi kidato cha nne lakini hakufanikiwa kufaulu vizuri na kujiunga na chuo cha uandishi wa habari cha TSJ na kuchukua Certificate na Diploma ya uandishi wa habari.

"Nawapenda sana wazazi wangu na familia yangu kwani wamekuwa ni faraja kubwa kwangu kwa kunishauri mambo mbalimbali ya kimaisha.

Namshukuru Mungu kwa kuniweka katika familia hii iliyokuwa na amani na yenye upendo kiukweli wazazi wangu ndio marafiki zangu, dada zangu, kaka yangu na hata wadogo zangu ni faraja yangu.

Wazazi wangu wamekuwa wakitusikiliza wanawe kwa kila kitu na kutusaidia kadri ya uwezo wao na hata kutushauri pale wanapoona hapafai na ndio maana hadi sasa nimekuwa hivi nilivyo huku nikiendelea kupata ushauri wao kila nlipo uhitaji, 'MUNGU ZIDI KUWAHIFADHI WAZAZI WANGU WAZIDISHIE KHERI NA BARAKA'"

Start a discussion with Mwali ibrahim

Start a discussion