Sendi matiti
ASILI, KOO, DESTURI NA UTAMADUNI WA WANGOREME
Kabila la wangoreme limeundwa na watu waliotokea Arusha, Kenya na watu wa kusini mashariki ya tarafa ya ngoreme kufatana na historia iliyopatikana watangulizi wa kuingia ardhi ambayo sasa inaitwa ngoreme ni watu wa ukoo wa wamaare waliotokea Arusha kwa kabila la wasonjo. Badae walifatiwa na watu wa ukoo wa wataboori pia kutoka Arusha wakiwa na koo mbili za waihindi na wabugasa na asili yao walikuwa wawindaji zaidi . Kundi la pili lilikuwa watu kutoka Kenya wengi wao wana asili ya kikurya kwa vile walipitia ukuriani. Koo za watu hao zilikuwa kama zifatavyo; Wagiseero waliotokea Gisero Kenya na waliamini chui Wagoosi waliotokea Goosi , Kenya Wagitare walitokea Geitare Kenya Wairegi kutoka Bwiregi kaskazini mwa mto Mara Koo zingine kutoka eneo hilo ni za wa Wabusawe Wasweta Waraguuri Watimbaru Wanyabasi Kundi la tatu ni watu waliotokea ikizu ambao walikuja kuunda koo za wagimenye na wabwiro. ASILI YA WANGOREME NA UHUSIANO KATI YA WANGOREME NA WAIKOMA: Chanzo kingine cha habari kinaeleza kuwa waanzilishi wa kabila la wangoreme ni shujaa aliyeitwa Magwesi aliyetokea Regala Sanjo karibu na Loliondo. Magwesi aliyekuja na damu ya kimasai waliokuwa wanaitwa Sonjo. Mtatiro Nyigana Mkare aliwahi kufika Sonjo na kuelezea kuwa wasanjo wana lugha inayofanana na lugha ya kingurimi kwa maneno mengi Mzee magwesi aliamua kuhama Regata na mkewe na kwenda sehemu itwayo Manyare. Alipokuwa Regata alifanikiwa kupata watoto aliyekuwa wa kiume wa kwanza akamwita Waudira wa pili wa kiume pia akamwita Mwikoma na motto wa tatu Mogosuhi aliyekuwa wa kike. Ukoo wake ulizidi kupanuka akiwa manyare na alifia eneo hili hili Baada ya Mzee Magwesi kuaga dunia aliwachia madaraka mwanae Wandira ambae aliamua kuhamishia familia yao sehemu ya kijito itwayo Manchira. Inaasemekana mwikoma alipenda sana sehemu hiyo ilikuwa na wanyama wengi kwa vile alikuwa mwindaji. Ndio maana waikoma wako eneo hilo hadi sasa wakiwinda.Hata hivyo Wandira aliyekuwa mkulima hakupenda sehemu hiyo ya manchira kwa vile kulikuwa na wanyama wengi walioharibu mazao yake. Kwa hiyo Wandira aliamua kuhama na dada yake Mogosuhi na kumwacha mwikoma Wandira alihamia ikorongo akiwa na watoto wengi akiwemo mkubwa aliyeitwa motto mkubwa aliyeitwa Sabayaya Baada ya Wandira kuaga dunia sabayaya alishika madaraka ya familia naya sabayaya alipata watoto wengi akiwemo mtoto wake mkubwa aliyemwita Mongoreme. kijana mongoreme aliyeshika madaraka alikabiliwa na matatizo mengi likiwemo tatizo la kushambuliwa na wamasai mara kwa mara na hivyo kuamua kuhamia sehemuambayo angetengeneza kinga dhidi ya maadui obori. Sohemu hiyo ilikuwa ni bonde lilozungukwa na vilima vine vya magange, kibairemera, nyangekenge na kewaigenga ambapo ilikuwa ni rahisi kuziba milango mitatu iliyopo naye Mugusuhi alihamia Kenya na kuolewa huko.
Mangwesi
Mwaikoma
Wandhira
Mogusuhi Sabayaya Mongoreme
Msaai
Kwa watu wenye umri mkubwa bila shaka waliwai kusikiamisemo kama vile “Isabayaya ne wandira” wakiwa na maana kuwa Isabayaya mwana wa wandira na pia “Ngoreme ya Isabayaya” wakiwa na maana Ngoreme mwana wa Isabayaya. Aidha kuna matumaini yaliyokuwa yakisikika kama “Ngoreme wa Nyahaba” ikiwa na uwezekano kuwa nyahaba huyo alikuja baada ya Mongoreme
13.2 KOO, MILANGO YA WANGOREME NA ALAMA ZAO ZA KUAPIA
Baada ya kuzaliana na kuongezeka wangoreme waligawanyika katika milango mbalimbali na kuwa na alama za kuapia kama ifatavyo
I, Wagoosi kutoka Kenya kupitia ukuriani – Ng’ombe na brashi
Ii, Wagisero kutoka gisero, ukuriani – Ng’ombe
Iii, Wabugasa kutoka sanjo – Fisi
Iv, Waihindi kutoka sanjo – Fisi
V, Wamaare kutoka sanjo Sanjo – Ng’ombe na Nyani
Vi, Wagitare kutoka gitare – Samaki
Vii, Wabwiro kutoka ikizu –Makoome Na kunde
Viii, Wairegi kutoka Bwiregi- Ng’ombe Na Nyama
Ix , Wagimenye kutoka ikizu
X, Wanguku kutoka umasaini – Sarota
Xi, Wabusawe
Kama ilivyoelezwa hapo awali, milango au makundi mengine yaishio ngoreme ni ya wasweta waraguuri, watimbaru na wanyabasi. Kwa upande wa arama watangulizi (wazee) wangoreme waliziweka ili yeyote atakayeapa kwa uongo mji wake upate matatizo.
13.3 Makundi Ya Kishujaa Ya Wasaai Na Wachuma Wangoreme pia waligawa koo zao kwa makundi mawili katika kuashiriaushujaa. Makundi hayo ni Wasaai kutokana na jina la mtoto wa kiume wa mongoreme aliyeitwa masaai Wasaai Wachuma Abagisego Abarimbare Ababugasa Abagaasi Ababusawe Abairege Abagitare Ababwiro Ababutacha Abaihindi Abamare Abanguku Abagimenye Abakombo Abaraguri 13.4 Makundi Ya Kirika Kulikuwa na makundi mengine ya kirika ambayo kwa kingoreme yalijulikana kama amakora. Rika hizo kwa upande wa Wasaai na Wachuma ni kama zifatazo Wasaai Wachuma Abasaai Abachuma Abamaina Abanyangi Abagamunyari Abagini Abanyambureti Abamairabe Rika hizo zilienda Kwa mzunguko moja baada ya mwingine kwa mfano Abachuma mzunguko upo kama ifatavyo.
Abachuma Abanyangi
Abamairabe Abagini
Pia kulikuwa Na makundi mengine yanayojulikana Kwa lugha ya kingoreme Kama Chisaga Kama ifatavyo
• Wasaai walikuwa na “chisaga” za Bongirate na Romore • Wachuma walikuwa na chisaga za Borimarancha na Gamuntenya.
13.5 Miezi ya Wangoreme
Hapo zamani wangoreme hawakuwa na utaratibu wa kuhesabu miezi kama ilivyo siku hizi yaani Januari, Februari……… Hadi Desemba. Badala yake waliweza kuhesabu miezi yao kufatana na majira ya kilimo kama ifatavyo
1, Itaturi—Matorora (Mashamba yaliyovunwa)yanaanza kuota majani (yaraitaroora)
2, Itabarari --- wawindaji wanawinda
3, Kimaga – mwezi ambao mvua hainyeshi, kwa hiyo unawake kwa uwazi zaidi
4, Kemwamuya ya mbele (I)—Mwezi unakuwa mweusi kwajili ya kutanda mawingu ya mvua.
5, Kemwamu ya kabere (II) ---
6, Kirabu (I) ---Mvua nyeupe sio nzito
7, Kirabu (II) ---- kwendelea kwa kirabu
8, Nyamabeho --- Mwezi wa baridi
9, Nyansahi – Mwezi baada ya mvuno, sherehe, saro, kutembeleana
10, Rungaka—Mmea aina ya “rugaka” umeanza kutoa maua.
11, Tiiri – Kilimo kuanza na kupanda mazao
12, Kinyariri --- Majani yaliyochomwa yanaota upya
SIMULIZI ZINAZOHUSU KOO ZA ABAHIRI MATITI NA ABAHIRI MKARE
hariri1. “Ubalozi” wa abahiri Mokiri sehemu ya Burumarancha.
Kufuatana na maelezo ya mzee Fanuel Makuru Nyaborimani, abahiri Mokiri walipendelea kuishi sehemu ya Burumarancha hata baada ya kuhamia eneo la Nguku. Ili kujua iwapo watu wa Burumarancha walikuwa wakiwasema vizuri au vibaya abahiri Mokiri, kijana Mkare kutoka Nguku alitumwa huko Burumarancha ili awe “balozi” au mchunguzi kuona iwapo abahiri Mokiri walikuwa wakisemwa vizuri. Inasemekana kuwa Mzee Mkare alifia huko Burumarancha baada ya kuwazaa watoto wawili, Nyigana na mtoto mwingine. Baada ya kufiwa na baba yake, kijana Nyigana aliamua kuwafuata watu wa ukoo wake huko Nguku. Mzee Fanuel anasimulia kuwa Mzee Nyaborimani ndiye alimsaidia Nyigana kuwatafuta wana ukoo wake hao na hatimaye kumpata Kemriho Muhoni ambako Nyigana aliamua kuishi naye. Hata hivyo kutokana na hamu ya Abahiri Mokiri kuishi huko Burumarancha, mtoto wa Nyigana aitwaye Mtatiro alitumwa huko ili awe “balozi” wao. Kinyume na matakwa ya Abahiri Mokiri kuwa na balozi wao huko Burumarancha, kijana Mtatiro hakuweza kuishi huko alirudi Nguku kwa Abahiri Mokiri wenzake. Kizazi cha sasa kinadhania kuwa huenda kuhamia Sang’anga kwa mjukuu wa Nyigana aitwaye Wambura Mokiri Nyigana mwaka 2010 ni mwendelezo wa tamaa ya Abahiri Mokiri kuwa na “balozi” wao huko Burumarancha, hata kama jambo hilo halikupangwa hivyo. Ndugu Makuru Nyaborimani anasimulia kwamba Mzee Nyaborimani ndiye aliyetekeleza mchakato mzima wa uchumba wa Nyigana Mkare kwa Esta Nyabakara Charwe Sura. Aidha inasimuliwa kuwa kutokana na Mzee Charwe Sura kuwa na kijana mdogo wa kiume aitwaye Matiti, Nyigana Mkare aliombwa na kukubali kujenga karibu na baba mkwe wake Charwe awe kama kijana wake wa kiume (omomura) wa kumlinda na kumsaidia kazi.
2. Kuuawa kwa Charwe Wambura na asili ya jina la mwanae Geteba
Mchungaji F. Makuru Nyaborimani anasimulia kuwa hapo zamani Mzee Charwe Wambura wa Nguku aliweza kuvuna chakula tele na kujaza maghala wakati sehemu nyingine ikiwemo Bisegeso wakilia njaa. Inasemekana kuwa vijana fulani wa Bisegeso walimwendea Mzee Charwe na kumuomba awapatie chakula na walipokataliwa vijana hao siku moja waliamua kumvizia na kumuua Mzee Charwe kwa kumpiga mshale wa sumu kutokana na hasira zao na kutokomea na chakula. Inaelezwa kuwa wakati akikaribia kukata roho, Mzee Charwe alitoa wosia kuwa mke wake aliyekuwa na mimba wakati huo akizaa mtoto amwite “Geteba” badala ya kuitwa Masirori, jina ambalo hapo awali alipanga kumuita. Alitaka mtoto wake aitwe “Geteba” kwa tafasiri ya lugha kingoreme “tukio lisilosahauliwa”. Inasimuliwa kuwa tukio hilo la kikatili liliweza kujenga uadui mkubwa kati ya wakazi wa Bisegeso (ababisegeso) na wakazi wa Nguku (abanguku).
3. Asili ya majina ya abahiri Matiti na abahiri Saroti
Inasimuliwa kuwa hapo zamani kulikuwepo na mzee mmoja aliyekuwa mkulima aitwaye Isabosi Matiti. Inasemekana kuwa siku moja Isabosi wakati wa kuwasha moto katika makazi yake karibu na kisima chake alichokianzisha cha Kiru, moshi wa moto wake uliweza kuonekana kwa mbali na mtu mwingine aitwaye Saroti aliyekuwa mwindaji wanyama na aliyekuwa akiishi Gisena. Saroti maisha yake yalikuwa ya porini, akiwinda na kula matunda pori na hakujua chochote kuhusu kilimo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa kutokana na jina lake na aina ya maisha yake mtu huyo alitokea Sonjo, mkoani Arusha. Siku moja Saroti baada ya kuona moshi ukifuka aliamua kuufuatilia kujua kuwa ni nani aliyekuwa anaishi huko, waweza kufahamiana. Ili asipotee njia aliyopitia wakati wa kurudi kwake, Saroti aliweka alama ya njia aliyopitia kwa kuvunja vijiti. Baada ya Isabosi na Saroti kukutana na kufahamiana, Saroti aliomba apewe mojawapo wa mabinti wawili wa Isabosi ili aweze kumuoa. Inasemekana kuwa binti mkubwa alikataa kuolewa na Saroti kwa vile huyo mwindaji alikuwa mchafu, mwenye nywele zinazonuka na alikuwa hajui kuoga vizuri. Kuoga kwake kulikuwa ni kujitumbukiza kwenye dimbwi la maji huku akiinua juu mikono yake yote miwili, mkono mmoja ukishikilia mishale na mkono wa pili akishikilia upinde, kwa njia ya kujihami wakati wote iwapo atashambuliwa na adui.
Binti mdogo wa Isabosi yeye alikubali kuolewa na Saroti lakini kwa masharti yaliyotolewa na mzee Isabosi kuwa itabidi Saroti awe msafi kwa kunyolewa nywele na kujua jinsi ya kuoga vizuri.
Saroti alikubali kunyolewa nywele lakini katika kukabili maumivu ya kunyolewa kwa kisu, alipewa mtama mtamu uliopikwa vizuri ili atafune wakati akinyolewa. Pia Saroti alipelekwa mtoni na kufundishwa jinsi ya kuoga vizuri. La kushangaza ni kuwa Saroti pia ilibidi afundishwe namna ya “kupata mtoto” kwa vile inasemekana katika maisha yake yote alikuwa hajawahi kukutana na mwanamke kiunyumba. Baada ya Saroti kuoa kwa Isabosi, alianzisha ukoo unaojulikana sasa kama abahiri Saroti na Isabosi naye aliendeleza ukoo wa abahiri Matiti. Inasemekana kuwa koo hizo mbili ndizo zilikuwa kubwa sana sehemu ya Ngoreme wakati huo.
4. Njia iliyotumika kuhesabu siku hapo zamani
Inasimuliwa kuwa hapo zamani siku za wiki yaani Jumatatu, Jumanne, Jumatano hadi Jumapili hazikuwepo wala tarehe za kalenda zilizopo siku hizi hazikufahamika kwa hiyo iwapo mtu alitaka akutane na mwenzie alitamka kuwa kwa mfano wakutane siku ya sita kuanzia kesho yake. Ili aweze kufuatilia vyema hesabu ya siku mtu huyo aliweka mafundo ya kamba sita na kufungua fundo moja baada ya lingine kwa kadri siku zinavyopita.
5. Asili ya majina ya baadhi ya maeneo ya Ngoreme na watu binafsi
Yafuatayo ni asili majina ya baadhi ya maeneo ya Ngoreme na ya watu binafsi pia:
5.1 Buchanchari Eneo la Buchanchari ilipo shule ya msingi ya Buchanchari, kijiji cha Buchanchari kata ya Kisaka hapo zamani jina lake la asili ni Nyatontobe. Eneo hilo la Nyatontobe lilipewa jina la Buchanchari kutokana na kuzagaa malishoni kwa kondoo wa tajiri mmoja wa mifugo aliyeishi hapo zama hizo. “Kuchanchara” ni neno la kingoreme ambalo tafasiri yake kwa lugha ya Kiswahili ni kuzagaa au kusambaa. 5.2 Nyabehore Nyabehore, eneo ambalo kwa hivi sasa kuna shule ya sekondari ya Nyabehore, kijiji cha Gantamome, Ngoreme ni jina lililopewa eneo hilo kukumbushia tukio la kuzagaa kwa vichwa vya watu kutokana na vita iliyopiganiwa hapo kwa wakati fulani. Nyabehore ni neno la kingoreme ambalo tafasiri yake kwa lugha ya Kiswahili ni kwenye au penye vichwa. 5.3 Asili ya jina “Nyigana”
Nyigana ni jina alilopewa mtoto wa Mkare Kitege ambaye jina lake hasa ni Burwe. Alipewa jina hilo kutokana na jina la babu yake ambaye alikuwa tajiri wa ng’ombe na hivyo kupewa jina la tambo la Nyigana re ng’ombe (Ng’ombe mia). Nyigana Mkare mwenyewe hakuwa tajiri.
5.4 Nyimata kuitwa “Nyamakohe”
Mzee Wambura Nyimata alikuwa akiitwa “Maro Nyamakohe Laki”. Hii ni kutokana na utajiri mkubwa wa ng’ombe aliyokuwa nao mzee Nyimata Gesya na hivyo mwanae kuitwa “mwana wa Nyamakohe laki”. Amakohe ni neno la kingoreme likiwa na tafsiri ya Kiswahili ya ndama wakubwa.
5.5 Nguku
Jina “Nguku” inasemekana linatokana na neno la kikurya ambalo lina maana ya “kilima”. Inasimuliwa kuwa hapo zamani sana mkurya upande wa pili wa mto Mara katika kumuelekeza mwenzake ndugu yao alipoenda au kuhamia alisonda kidole na kusema “amekwenda katika kilima kile” au kwa maneno ya kikurya “ageye konguku eera”. Kilima kilichokuwa kikisemwa ni cha Gisena kilichopo sasa eneo la Nguku, Ngoreme.
5.6 Machegechege
Maana yake ni aina fulani ya miti iitwayo “EBITAMANKWE” iliyokuwa eneo hilo ambayo huzaa aina fulani ya matunda marefu kadri ya futi moja ambayo ndani yake kuna mbegu safu mbili, ambayo yakikauka ukiyatikisa hulia chege, chege. Basi Wangoreme wakasema hapa ni kwenye Machegechege.
5.7 Kobetimo Ebetimo kwa Kingoreme ni Makurwiri: eneo hilo lina Kakurwiri mengi hivyo Wangoreme wakasema hapa ni Kobetimo. 5.8 Nyansurumunti Ebesurumunti ni wadudu fulani wadogo, ambao husumbua sana kwa kuzunguka zunguka na kutaka kuingia masikioni wakipiga kelele. Wadudu hao ni wasumbufu sana. 5.9 Ganora Ganora maana yake “ YAMENENEPA” jina hilo lilitokana na watu katika kitongoji hicho kunenepa wanaume kwa wanawake. Sasa watu wakiwaona wanasema haya ni ya kule kwa yale yaliyonenepa “GANO NGA GANORA”. Hivyo mwishoe kitongoji kile kikaitwa Ganora. 6. Maeneo yenye maajabu Ngoreme
Kuna maeneo mengi yenye maajabu na kwa uhakika baadhi ya maeneo hayo yakiboreshwa yanaweza kuwa vivutio vya kitalii. Baadhi ya maeneo hayo ni kama yafuatayo:
6.1 Mangwesi
Katika eneo la Mangwesi karibu na Mugumu, mji mkuu wa wilaya ya Serengeti kuna mfano wa mafiga matatu, chungu, mwiko, moto usiozimika na kiti (aina ya kigoda) cha jiwe. Wenyeji wanaelezea kuwa mafiga matatu yanawakilisha makabila matatu ya Waikoma, Wangoreme na Wanata. Vilima vya Mangwesi na Manyara ndipo Wangoreme na Waikoma walitengana wakitokea Sonjo Arusha.
6.2 Majimoto
Tangu enzi za kikoloni, majimoto kimekuwa kijiji au kituo cha makao makuu ya tarafa ya Ngoreme. Hadi leo kuna kisima kinachofuka maji ya moto katika eneo hilo. Inaelezwa kuwa hapo siku za nyuma kisima hicho kilikuwa kinatoa maji ya moto sana kiasi cha kufanya dimbwi jirani kuwa chanzo cha maji moto ambayo yaliweza kutumika kuchemsha na kuivisha mahindi mabichi. Kutokana na maji kuwa na chumvi, mahindi hayo yaliiva na kuungwa kiasili kwa chumvi hiyo, tayari kwa kuliwa. Kuna maelezo ya aina mbili kuhusu chanzo cha maji hayo kuwa na joto na chumvi. Wazee wa zamani walielezea kuwa maji hayo yalitokana na mama kikongwe mmoja aliyekuwa ardhini, aliyekuwa anachemsha maji kwa kutumia chungu. Wanaeleza kuwa mama huyo alikuwa akitibua maji mara nyingi na hivyo kufanya maji moto kufoka na kutoka nje kwa vipindi vifupi vifupi. Hata hivyo wana sayansi wanaeleza kuwa kisima cha maji moto asili yake ni matokeo ya kivolikaniki (volcanic actions) ambapo joto kutoka ardhini hupitia katika nyufa za mawe na kufikia kisima cha maji na hivyo kuchemsha maji ya kisima hicho. Eneo la maji moto lina utajiri wa madini aina ya dhahabu na gesi yenye thamani kubwa. Kuna haja ya kuliendeleza ili kuleta maendeleo Ngoreme na nchini kwa ujumla.
6.3 Magena Mang’ore
Magena Mang’ore ni maneno ya kingoreme ambayo tafasiri yake kwa lugha ya Kiswahili ni mawe yenye michoro au maandishi. Baadhi ya watu wanasema kuwa maandishi hayo yapo katika lugha ya kirumi. Eneo lenye mawe hayo ni kijiji cha Gantamome Ngoreme. Kuna haja ya kulifanyia eneo hilo utafiti wa kina wa kihistoria na kijiolojia ili kugundua kuwa nani aliyachora na lini. Aidha kuna umuhimu wa kuhifadhi vyema eneo hilo ili liweze kuwa kivutio cha utalii hapo baadae.
6.4 Itacho rensoku
Itacho rensoku ni maneno mawili ya kingoreme yanayoweza kutafasiriwa Kiswahili kama “unyoya wa swala” katika eneo la Gantamome (Nyamehuru) kuna jiwe ambalo lina alama wazi ya unyayo wa mnyama funo. Kuna haja ya kulifanyia utafiti jambo hilo ili kama jiwe hilo litakidhi viwango vya kiutalii liweze pia kuwa kivutio cha utalii.
6.5 Wigo wa mawe wa kuzuia maadui
Katika kukabiliana na maadui wa kutoka nje, hasa wamasai, wangoreme walijenga maboma makubwa ya mawe ili waweze kujikinga wao wenyewe na mifugo yao. Wigo mkubwa upo hadi leo katika kilima cha Gisena na ulitumika kukinga jamii nzima. Katika kilima cha Genteme kitongoji cha Ganga, kijiji cha Buchanchari. Pia kulijengwa maboma manne ya namna hiyo lakini madogo ya watu binafsi ambao kwa majina ni Ikenge, kumba na Isanko. Kwa bahati mbaya maboma hayo manne karibu yanamalizika kutokana na mawe yake kusombwa na watu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba. Katika miaka ya hivi karibuni mzee Samson Wakibara wa Gantamome, Ngoreme pia alijengea familia yake boma kubwa la mawe ambalo lipo hadi leo.
"Mchoro ntaleta japokuwa wenyeji wa buchanchari kuna mlima gisena watakuwa wameshuhudia mawe yakiwa yamepangiliwa vizuri sana kuelekea kobori" Sendi Matiti Mokiri
Maboma hayo ya mawe ambayo kwa lugha ya kingoreme yanaitwa chebugo (au likiwa moja obugo) yanafaa kuhifadhiwa vyema ili yawe kumbukumbu ya kizazi cha leo na vile vijavyo na ikibidi kuwa vivutio vya kitalii.
6.6 Kisima cha Kiru
Kisima cha Kiru kilichopo kijiji cha Gantamome ni maarufu sana kwa ajili ya mitambiko ya Wangoreme eneo hilo. Kilikuwa kinasafishwa na kufanyiwa kafara za kuchinja wanyama. Inaelezwa na waliowahi kutambikia huko kuwa mara nyingi yalionekana maajabu wakati wa kufanya matambiko na kuombea heri kwa masuala mbalimbali kwa mfano kuonekana mbuzi mweupe na nyoka wa ajabu.
7. Ujio wa Wanyiramba
Kutokana na maelezo ya mzee Makuru Nyaborimani kabila la Wanyiramba waliwahi kupitia na kuishi Ngoreme wakitokea Tarime. Hii ndiyo sababu kuna sehemu ya Ngoreme iitwayo Iramba. Wanyiramba na Wangoreme ni watani wa jadi kwa vile walipigana vita. Aidha inaelezwa kuwa wakati wakiwa Ngoreme walitambikia jiwe sehemu ya Sang’anga.
8. Jinsi watoto wa Gesya Wambura walivyoathirika na tatizo la ugonjwa wa ndui
Kufuatana na maelezo ya mzee Geteba Charwe, watoto wa Gesya yaani Nyimata Gesya na Boke Gesya walipata shida sana baada ya baba na mama yao kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa ndui (oborondo) na hivyo kuwaacha yatima. Inaelezwa kuwa Nyimata Gesya alitunzwa na kuozwa na Charwe Wambura, ambaye ni kaka ya baba yao. Kwa taarifa ya msomaji, Charwe Wambura ndiye baba yake Geteba ambaye ndiye msimuliaji wa taarifa hii. Nyimata na Boke baada ya kuwa watoto yatima waliweza kukabiliana kishujaa na tatizo la njaa ambalo lilikuwepo wakati huo. Inaelezwa kuwa wote wawili waliwinda wanyama pori kwa ajili ya kitoweo na waliletewa ulezi na mzee Charwe Wambura na kwa kuogopa wasinyang’anywe chakula na watu wabaya, waliuficha ulezi katika ghala la ardhini ambalo waliliandaa kwa msaada wa baba yao mkubwa mzee Charwe Wambura.
9. Kisa cha jina la “Matiti” kupatikana kwa Ababusawe
Ababusawe ni watu wanaoishi Busawe Ngoreme. Inasemekana kuwa jina la Matiti pia kwa Ababisawe kutokana na hapo zamani Matiti Wambura alipoenda kuwinda aliwaua wanyama wengi sana lakini aliwanyima ndugu zake nyama pale walipomwomba. Kutokana na tabia yake hiyo ya unyimi ndugu zake walimchukia na kumsusia na hivyo Matiti Charwe ilimbidi kuhamia Busawe.
10. Kisa cha mzee Nyigana Mkare kuponea chupuchupu mara tatu kupoteza maisha.
Mzee Nyigana Mkare alisimulia kuwa katika ujana wake siku moja usiku alikamatwa kwa nguvu na askari kwa ajili ya kupelekwa kuwa manamba katika mashamba ya mkonge, yeye na wenzake walitekwa usiku na kusafirishwa hadi sehemu ya Kilimatinde, walipopumzika na kupata chakula. Wakati wa kupumzika Nyigana aliandaa mbinu ya kutoroka kwa kuomba aende kujisaidia vichakani na alipewa askari mwenye bunduki ampeleke kujisaidia. Walipofika huko Nyigana alimwomba ajisetiri kichakani kwa kusema: “Askari si visuri nikichorona unaniangalia kwetu ni mugiro”. Askari huyo alimkubalia ombi lake la kutaka kujisetiri. Lakini Nyigana alipokuwa kichakani alikurupuka mbio, askari akamkimbiza na kumfyatulia risasi ambayo bahati nzuri haikumpata Nyigana. Kwa kumpoteza askari alibidi Nyigana ajitumbukize katika korongo lililotandwa na kufunikwa na mimea inayotambaa, Kwa hiyo askari alishindwa kumpata. Hiyo ndiyo chupuchupu ya kwanza. Nyigana baada ya kumtoroka askari, alikimbia hadi usiku ukaingia. Kwa bahati nzuri akiwa amechoka sana huku usiku umeingia alikiona kibanda kupitia mbaramwezi huko porini na akaamua kuingia humo ambapo alikuta moto na akaanza kuota moto huo hata bila ya wakazi wake kuwepo kwa vile ilikuwa baridi sana. Lakini Lo! Alipotazama aliona kitoto kilicholala na huku kichwa chake kimegeuzwa kuelekea mekoni. Kwa hofu kubwa alitoka nje ya kibanda hicho na kuanza kukimbia, lakini hakufika mbali akawaona wanawake wawili wakiwa uchi wa mnyama wakikaribia kibanda hicho. Kwa wasiwasi lakini kwa kujikaza Nyigana aliwauliza kwa lugha ya kingoreme “Ninyu bahe?” yaani “nyie ni nani?” Nao wakajibu kwa kejeli “banyonyoko” yaani “sisi na mama zako”. Nyigana kwa kujibiwa hivyo alichomoka kwa kasi ya mshale na kuweza kuwatoroka wanawake wachawi hao. Hiyo ni chupuchupu ya pili. Katika kuendelea na safari hiyo usiku wa manane Nyigana aliweza kuona nyumba kwa umbali kwa vile ilikuwa mbaramwezi. Akashusha pumzi kwa faraja lakini alipokuwa anagusa mlango wa nyumba hiyo alisikia mtu akija kufungua mlango na kwa kuchukua tahadhari Nyigana akatamka kwa sauti kubwa “uhoni eni tende mobisa he” kwa lugha ya Kiswahili tafasiri ya maneno hayo ni “Niponyeni miye siye adui”. Mwenye nyumba akamjibu Nyigana kuwa una bahati sana kusema mapema kwa vile alikuwa na nia ya kummalizia mbali na mshale wa sumu. Mwenye nyumba alimwelezea Nyigana jinsi watu fulani walivyomsumbua usiku na hata kumchukulia mtoto wake mdogo. Alidhani watu hao ndiyo wamerudi tena. Hiyo ndiyo chupuchupu ya tatu.
11. Esta Nyabakara Charwe kutokewa na muujiza
Kufuatana na maelezo ya Geteba Charwe mama Nyabakara hata kabla ya kubatizwa aliwahi kutokewa na muujiza. Muujiza wenyewe ni kuwa siku moja akiwa msichana alipokuwa akitoka kuchunga sehemu ya Kobibanga – Nyamitegete, ghafla aliona nchi imetanda giza nene ajabu. Lakini huku akiwa bado ameshangaa na kuogopa, ghafla tena baada ya dakika kama tano hivi jua likaonekana tena na akaendelea na safari yake. Hata hivyo hakuulizwa iwapo watu wengine siku hiyo waliona hali hiyo au la ili kujenga hoja kuwa huenda lilikuwa ni tukio la kawaida la kupatwa kwa jua.
HISTORIA YA UKOO WA NYIGANA MKARE
haririKuzaliwa kwa mzee Nyigana
Hakuna anayejua tarehe kamili ya kuzaliwa kwa mzee Nyigana. Hata hivyo kwa vile wakati anamwoa Esta Nyabakara alikuwa na umri mkubwa, ikiwa ni ndoa yake ya pili inakisiwa alizaliwa mwishoni mwa karne ya 19 yaani miaka ya 1890s. Inaelezwa kuwa alizaliwa katika kitongoji cha Gisena –Kwimange, Ngoreme. Jina lake lingine alilopewa ni Burwe na jina la tambo za ujana ni “Gise keng’ombe omogini, eng’ombe ina omukandara”.
4.2 Tohara ya Ndugu Nyigana Mkare Inaelezwa kuwa Nyigana Mkare alitahiriwa mwanzoni mwa karne ya 20 katika eneo la Burumarancha kwa {egisero} liitwalo wakambuni 4.3 Ndoa
Esta Nyabakara alikuwa mke wa pili baada ya mke wa kwanza kuaga dunia. Mke wa kwanza alikuwa anaitwa Boke Nyaturuka ambaye alimzalia mtoto mmoja wa kiume. Lakini kwa bahati mbaya mke na mtoto wao waliaga dunia huko Magateni na kumuachia Nyigana maisha ya upweke. Mkosi mwingine ni kuwa kabla ya matukio hayo ya kusikitisha kutokea nyumba yao ilipigwa radi na kuungua kabisa. Baada ya hali hiyo kutokea, Nyigana akiwa katika umaskini alianza kukusanya nguvu ili aweze kuoa tena. Nyigana alihamia kijiji cha Nguku kwa mzee Kemriho Muhoni baada ya kuona kuwa sehemu alipoishi aliandamwa na mikasa na mikosi. Kutokana na hofu hiyo ya kukumbwa na mikosi Nyigana alienda ubugabo (mpiga ramli) kwa mjaluo ili kujinasua na matatizo hayo. Mjaluo baada ya kupiga ramli yake alimweleza Nyigana kuwa: “Ijapokuwa umeandamwa na mikosi hiyo na kukabiliana na umaskini inaonesha kuwa baadaye utapata watoto na wajukuu wengi na utajiri unaonekana katika uzao wako”. Katika harakati za kutafuta mali Nyigana aling’oa na kuuza mawe ya kusagia pamoja na kufanya biashara ya “ ebitogoro” (njuga). Shughuli hizo zilimwezesha kupata mbuzi 14. Aidha mzee Nyigana alisimulia kuwa kwa bahati alipata ng’ombe wawili waliopotea njia na hawakuwa na mwenyewe. Kwa kifupi alipata mbuzi 14 na ng’ombe 6 kuweza kumwoa mama Nyabakara Charwe Sura.
4.4 Dini
Mara nyingi Nyigana Mkare alihubiriwa ili ajiunge na kanisa la wasabato bila ya mafanikio. Mara ya kwanza alipoalikwa kuhudhuria sabato alikuja kanisani na wenzake ambao walibeba mikenge ya kunywea pombe ili baada ya sala waende zao kunywa pombe, Washiriki walishangaa sana kwa tukio hilo. Kwa vile kwao pombe ni haramu. Mzee Nyigana katika siku zake za mwisho wa maisha yake hakuweza kubatizwa ingawa kulikuwa na jitihada ya kufanya hivyo.
4.5 Karama na sifa za Nyigana Mkare
Mzee Nyigana katika maisha yake alikuwa na karama na sifa zifuatazo:
• Alikuwa mkarimu sana • Alikuwa mpole, asiyependa ugomvi wala uchokozi ijapokuwa alikuwa mwenye nguvu sana na mpiganaji mieleka wa kuogofya. • Alikuwa mtu aliyejali uhuru wa mtu kuamua mambo yake. Kwa mfano hakupenda kulazimisha watoto wake waoe miji ipi au wafanye kazi zipi, tofauti kabisa na wazazi wengine hasa katika enzi hizo. Hata hivyo alitoa ushauri kwa upendo na mafunzo. • Nyigana alijali sana kazi na alishauri watoto wake waoe wanawake wenye miili yenye nguvu na wachapa kazi. • Hakuwa na tabia ya unyanyasaji mke wake wala watoto. Mwandishi wa historia hii anashuhudia kuwa hakuwahi kuona Nyigana akimtukana au kumpiga mama yake Esta. • Nyigana mwenyewe alisimulia na wazee wengi wenye umri wake kutoa ushuhuda kuwa yeye alikuwa mtu mwenye miraba minne na mwenye nguvu nyingi sana. Nyigana alisimulia kuwa wakati wa ujana wake watu wawili waliokuwa wakisifika kwa nguvu ni yeye na mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Birage.
Wakati fulani yeye na Birage walitaka kupimana nguvu ili kujua nani zaidi, kati ya Birage aliyeweza kuzuia gari lisiondoke au Nyigana aliyeweza kunyanyua juu ng’ombe mzima. Kwa kawaida enzi hizo kabla ya watu kupimana nguvu kwa njia ya mieleka kipimo cha kwanza kilikuwa kushindana kuona ni yupi anaweza kula chakula kingi zaidi na kwa kasi kubwa. Siku ya mashindano kati ya Birage na Nyigana, viliandaliwa vyakula vingi na vya kila namna kisha vyakula hivyo kuwekwa kwa vyombo vya vyakula kwa mfano visonzo vikubwa viwili vya ugali vinavyolingana, vibuyu viwili vya togwa (obusera) vinavyolingana nk. Nyigana mwenyewe anasimulia kuwa shindano lilianza kwa wote kunywa togwa ambapo wote walimaliza vibuyu vyao kwa muda karibu sawa. Ikaja zamu ya kula ugali na nyama ambapo Birage alimega matonge 7 tu na kukausha kisonzo chake wakati Nyigana alikuwa bado anahangaika na kisonzo chake, ndipo wazee waliokuwa wasimamizi wa shindano hilo wakaamua kusimamisha shindano na kumshauri Nyigana asipigane mieleka na Birage, atammaliza, Kwa kuangalia wingi wa chakula anachoweza kula Birage
Kwa hiyo Nyigana na Birage walishikana mikono na kuacha shindano hilo kwa ajili ya kulinda heshima zao kwa maeneo walimoishi, Nyigana kaskazini mwa Ngoreme na Birage eneo la kusini. Inaelezwa kuwa kwa upande wa Birage mtoto aliyerithi nguvu zake alikuwa wa kike ambaye aliweza kuwatia adabu wanaume waliomwoa na hivyo kuachika na kuhamia sehemu ya Ikizu. Kwa upande wa Nyigana hakuweza kupata mtoto aliyechukua nguvu zake, labda kwa umbali Elias Nyigana aliyekuwa mpiga mieleka hodari lakini mwenye mwili mdogo na pia mjukuu wake aitwaye Nyamhanga Mokiri Nyigana aliye na mwili mkubwa aliyezaliwa na mama Kabe, mke wa Mokiri. Sura Nyigana akiwa shule ya msingi Kisangwa, akiwa kiranja mkuu mwaka 1960 aliwahi kupigana mieleka na pande la mtu lililokuwa likitamba huko na kuweza kulinyanyua juu kwa juu na kulitupa chini kwa kishindo kikubwa kilicholifanya mtu huyo kutapika maziwa aliyokunywa siku hiyo.
4.6 Ukoo na uzao wa mzee Nyigana Mkare
Maelezo kwa kirefu juu ya ukoo na uzao wa mzee Nyigana yapo katika viambatisho A na
C.
Nyigana alizaliwa kwa ukoo wa Abahiri Mkare. Inaelezwa kuwa muanzilishi wa ukoo huo (omusemori) anayefahamika ni Wikobiro. Mtiririko wa uzao ni kuwa Wikobiro alimzaa Mahe, naye Mahe alimzaa Ng’ochani aliyemzaa Mkare. Mzee Mkare baada ya kumuoa Moronge alimzaa Mokiri. Watoto 13 wa Mokiri kutokana na wanawake wane aliowaoa majina ya ni kama yafatayo
• Mke wa kwanza mama Nyamahemba aliwazaa Nyambura, Mesima, Kitege, Mresi na Kabuni. Nyigana Mkare alitokana na mlango wa Kitege Mokiri (tazama mchoro namba 8 hapo chini). • Mke wa pili wa Mokiri aliyeitwa Nchango aliwazaa Sarigoko, Kisaka, Mhoni na Sebe. • Mke wa tatu kwa jina Nyamoturi alizaa mtoto aliyemwita Mwita Mokiri. • Mke wa nne aliyeitwa Mkami naye aliwazaa Mambe, Torore na Manoga.
Mchoro namba 8: Ukoo na uzao wa mzee Nyigana Mkare
Kwa upande wa uzao, kama ilivyo katika maelekezo ya mwenziwe mama Esta, Nyigana alizaa jumla ya watoto 10 na kufikia Machi 2010 uzao wa Nyigana ulikuwa umefikia wajukuu 58, vitukuu 218 na vilembwe 23 waliokuwepo.
Wajukuu na vitukuu waliopewa jina la nyigana
Kama ilivyokuwa kwa mama Nyabakara, jina la mzee liliweza kupewa wajukuu na vitukuu wake kama ifuatavyo:
1. Wajukuu wake, Nyigana Mokiri kwa mama Ihumbwe, mama Kabe kwa mama Nyamhanga na mama Boke. Pia kuna Nyigana Mtatiro. 2. Kwa upande wa vitukuu ni: • Nyigana Jumanne Mtatiro • Nyigana Machumbe Maro (Kwa Mkami Mokiri). • Nyigana Ng’ochani Mokiri • Nyigana Mwita Mokiri (kwa karo) • Nyigana Mkongori Mokiri • Nyigana Kitege Mokiri • Nyigana Matiti Mokiri • Nyigana Maige Mokiri • Nyigana Moronge Mokiri • Nyigana Mkare Mokiri • Nyigana Bototo Nyamotwe • Nyigana Charwe • Nyigana Wambura Mokiri 4.7 Mzee Nyigana kuheshimu Sabato
Mzee Nyigana aliweza kuhubiriwa sana na waumini wa kanisa la Wasabato akiwemo mwenzi wake mama Esta Nyabakara. Hata hivyo alikuwa mgumu sana kuingia kanisa hilo kutokana na kunywa pombe. Kwa taarifa ya msomaji, pamoja na Nyigana kutokuwa katika dhehebu la wasabato yeye hakuwa kikwazo kwa mwenzi na watoto wake kuabudu dini hiyo ikiwa ni pamoja na kuacha kufanya kazi siku ya sabato. Mama Esta aliwahi kusimulia kuwa ni siku moja tu ambapo Nyigana alipomuomba Esta amsaidie kazi ya shamba siku ya jumamosi, kinyume na imani ya dini hiyo. Inasemekana kuwa sehemu waliopanda ulezi siku hiyo ya sabato, ulezi haukuweza kuota hapo. Tangu wakati huo mzee Nyigana aliogopa na kuheshimu siku ya sabato na hakuomba tena msabato yeyote amsaidie kazi siku hiyo ya ibada.
4.8 Kuugua na kuaga dunia kwa mzee Nyigana Mkare
Mnamo mwaka 1973 mzee Nyigana aliugua tumbo na ilibidi apasuliwe huko hospitali ya mwadui shinyanga alipokuwa anafanya kazi mwanae Elias Sura. Inaaminika kuwa chanzo cha kifo chake ni tatizo hilo na inasemekana kuwa baada ya kupata operesheni na kurudi kwake Ngoreme hali yake ya kiafya haikuweza kutengamaa kutokana na kutofuata masharti aliyopewa na daktari wa mwadui. Kutokana na kupenda kazi watu wanaeleza kuwa alianza kufanya kazi ngumu na kutozingatia masharti mengine aliyopewa. Mzee Nyigana Mkare aliaga dunia tarehe 13/03/1973 katika eneo la Marembota, kijiji cha Buchanchari. Inaelezwa kuwa Nyigana Mkare hakuwa na dada wala kaka au ndugu. Aidha wakati anazaliwa baba yake, mzee Mkare Kitege alikuwa ameishafariki dunia. Aliacha mke wake ana mimba na cha kusikitisha ni kuwa mama yake Nyigana aliyeitwa Kigocha alizaa watoto 10 na kati ya hao ni Nyigana pekee aliyekua hadi utu uzima. Watu wengine walimfahamu kwa jina la Nyigana Kigocha kutokana na kukuzwa na mama kigocha.