Makao makuu ni mahali ambako kuna ofisi kuu au uongozi wa taasisi, kampuni, shirika au mamlaka fulani. Mara nyingi ni jengo fulani kwa mfano jengo la Umoja wa Mataifa mjini New York penye ofisi ya Katibu Mkuu wa UM, ofisi za makatibu zake na ukumbi wa mikutano ya Mkutano Mkuu na Baraza la Usalama la UM.

Makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Mara nyingi ofisi za makao makuu ya shirika au mamlaka haziko mahali pamoja kijiografia lakini hata hivyo mikono yote ya uongozi kwa jumla huweza kuitwa "makao makuu".