Katibu Mkuu wa UM
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni mtendaji mkuu wa UM na mwenyekiti wa Ofisi Kuu ya UM ambayo ni kati ya vitengo muhimu vya Umoja wa Mataifa.
Uteuzi wa Katibu Mkuu
haririKatibu Mkuu huchaguliwa na Mkutano Mkuu wa UM kwa muda wa miaka mitano. Jina linapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu na Baraza la Usalama la UM. Kwa hiyo uteuzi wa Katibu Mkuu uko mkononi mwa Baraza la Usalama na kila taifa mjumbe wa kudumu linaweza kuzuia jina fulani lisipelekwa kwa njia ya Veto yake. Lakini Baraza la Usalama linapaswa kumteua mtu atakayepata kura za kutosha katika Mkutano Mkuu.
Hakuna sheria juu ya muda wa kazi yake lakini hadi sasa hakuna Katibu Mkuu aliyehudumia UM zaidi ya vipindi viwili au miaka 10. Kuna kawaida ya kwamba nafasi ya Katibu Mkuu inapita kwenye mabara yote ingawa hiyo si sheria.
Mshahara wa Katibu Mkuu ni dolar za Marekani 176,877 kwa mwaka. (2006).
Orodha ya Makatibu Wakuu
hariri# | Picha | Jina | Muda wa ukatibu wake |
Taifa lake | Mengineyo | Viungo |
---|---|---|---|---|---|---|
Gladwyn Jebb | 24 Oktoba 1945 – 2 Februari 1946 |
Uingereza | kaimu Katibu Mkuu | |||
1 | Trygve Halvdan Lie | 2 Februari 1946 – 10 Novemba 1952 |
Norwei | alijiuzulu | Biografia | |
2 | Faili:Dag Hammarskjold.jpg | Dag Hammarskjöld | 10 Aprili 1953 – 18 Septemba 1961 |
Uswidi | alikufa katika ajali ya ndege yake huko Rhodesia ya Kaskazini (leo Zambia) | Biografia |
3 | Sithu U Thant | 3 Novemba 1961 – 31 Desemba 1971 |
Burma (leo Myanmar) | kazi ya tar. 3 Novemba 1961 hadi 30 Novemba 1962 kaimu Katibu Mkuu | Biografia | |
4 | Kurt Waldheim | 1 Januari 1972 – 31 Desemba 1981 |
Austria | Veto ya China ilizuia kipindi cha tatu | Biografia | |
5 | Javier Pérez de Cuéllar | 1 Januari 1982 – 31 Desemba 1991 |
Peru | hakugombea mara ya tatu | Biografia | |
6 | Boutros Boutros-Ghali | 1 Januari 1992 – 31 Desemba 1996 |
Misri | Veto ya Marekani ilizuia kipindi cha pili | Biografia | |
7 | Kofi Annan | 1 Januari 1997 – 31 Desemba 2006 |
Ghana | hakugombea kipindi cha tatu | Biografia | |
8 | Ban Ki-moon | 1 Januari 2007 – | Korea Kusini | Biografia |
Makamu wa Katibu Mkuu
haririMkutano Mkuu uliamua 1997 kuanzisha cheo kipya cha makamu wa Katibu Mkuu.
Tangu 7 Januari 2007 Asha-Rose Migiro kutoka Tanzania amepewa nafasi hii. Alimfuata Mark Malloch Brown.