Make A Difference (MAD) Now
Make A Difference (MAD) Now ni shirika lisilo la faida ambalo linatoa elimu bora na mafunzo ya ajira na kujiajiri kwa vijana na wanawake wenye mahitaji nchini Tanzania pamoja na Amerika ya Kusini.Shirika hili limesaidia maelfu ya vijana nchini Tanzania na Amerika ya Kusini kupata elimu bora. Pia limesaidia kujenga shule na vituo vya ufundi katika jamii. Shirika la MAD lilianzishwa mnamo mwaka 2008 na Theresa Grant ambaye alikuwa na wito wa dhati wa kuleta mabadiliko ulimwenguni.[1]
Historia
haririTheresa Grant alitoka Amerika na alihamia Afrika baada ya kuuza kila kitu alichokuwa nacho nchini Amerika na kuja Afrika na kuanza kupeleka watoto katika shule za serikali nchini Zambia. Hata hivyo, alihitaji kufanya mengi zaidi ili kuboresha maisha ya watoto hao.[2]
Baada ya kuzungumza na wenyeji nchini Zambia, alijifunza kuwa elimu bora ni muhimu kwa kuwasaidia kuepukana na umaskini uliopitiliza. Katika miaka ya hivi karibuni shirika la MAD Now limeongeza programu nyingine inayolenga mafunzo ya ajira na kujiajiri kwa vijana na wanawake wenye mahitaji. Mpango huu umekuwa endelevu zaidi kwa ukuaji na umesaidia wanawake wengi na vijana kujitegemea.
Marejeo
hariri- ↑ "Kuhusu mad now". kuanzishwa 2008). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-11-26. Iliwekwa mnamo 2023-11-26.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ "Shirika hili limesaidia maelfu ya vijana nchini Tanzania na Amerika ya Kusini kupata elimu bora". 2008-2023).
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |