Makongolosi

(Elekezwa kutoka Makongorosi)

Makongolosi ni kata ya Wilaya ya Chunya katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania.

Makongolosi kwa sasa ni mamlaka ya mji mdogo ndani ya Wilaya ya Chunya. Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 23,787 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,116 [2] walioishi humo.

Makongolosi ni kati ya miji mipya iliyoanzishwa hivi karibuni (mwaka 2011), kwa hiyo ni mji ambao ni mchanga lakini ni kati ya miji inayokua kwa kasi katika Mkoa wa Mbeya, ambapo kwa sasa ina wakazi wa makabila tofautitofauti kutoka karibia kila pembe ya Tanzania.

Wakazi wake wanajihusisha na machimbo ya dhahabu, pamoja na biashara mbalimbali za mazao ya shambani, mazao ya wanyama, na pia biashara za bidhaa za viwandani.

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Chunya DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-29.
  Kata za Wilaya ya Chunya - Tanzania  

Bwawani | Chalangwa | Chokaa | Ifumbo | Itewe | Kambikatoto | Kasanga | Lupa | Lualaje | Mafyeko | Makongolosi | Mamba | Matundasi | Matwiga | Mbugani | Mkola | Mtanila | Nkung'ungu | Sangambi | Upendo


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Makongolosi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.