Makubaliano ya Kimataifa juu ya Haki za kiraia na kisiasa

Makubaliano ya Kimataifa juu ya Haki za kiraia na kisiasa ni makubaliano ya wadau wa haki za Kiraia na za Kisiasa kimataifa yaliyokubaliwa na mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Azimio 2200A (XXI) mnamo tarehe 16 Disemba 1966 na utekelezaji ulianza machi 23,1976 kulingana na kifungu cha 49 cha makubaliano. Kifungu cha 49 kinaruhusu makubaliano kuingia au kuanza utekelezaji miezi mitatu tangu tarehe ya kuwekwa sahihi na wawakilishi 35. Makubaliano yanataka washirika kuheshimu haki za kiraia na za kisiasa za watu zikiwa ni pamoja na haki ya kuishi, uhuru wa kuabudu, uhuru wa kuzungumza, uhuru wa kukusanyika na haki ya kuchagua, haki ya kusikilizwa na haki ya kimahakama. [1] [2]

Marejeo

hariri
  1. International Covenant on Civil and Political Rights Office of the United Nations High Commissioner of Human Rights
  2. "OHCHR Dashboard". Status of ratification{{cite web}}: CS1 maint: url-status (link)