Manchuria
Manchuria ni jina la kihistoria kwa eneo katika kaskazini-mashariki ya China. Leo hii limegawiwa katika majimbo ya Heilongjiang, Jilin na Liaoning.
Kabla ya 1858 maeneo ya Siberia ya kusini-mashariki ng'ambo ya mto Amur yalihesabiwa pia kuwa sehemu za Manchuria zikatwaliwa na Urusi. Wachina huiita "Manchuria ya Nje".
Watu wa Manchuria walitawala China mara kadhaa. Nasaba ya Qing yenye asili ya Manchuria ilitawala China kuanzia 1644 hadi mwisho wa milki ya China mwaka 1911.
Kati ya 1931 na 1945 Manchuria ilikuwa nchi lindwa iliyosimamiwa na Japani kwa jina la "Manchukuo" iliyorudishwa kwa China baada ya vita kuu ya pili ya dunia.