Siberia (kwa Kirusi: Сиби́рь, Sibir; kwa Kitartari: Seber) ni eneo kubwa mashariki mwa Urusi. Ni zaidi ya nusu ya eneo la Urusi wote. Eneo lake lote ni kilomita za mraba milioni 9.6 ambayo ni karibu sawa na Ulaya yote (km² milioni 10.6).

Eneo la Siberia: nyekundu yote; Jimbo la Siberia ndani ya shirikisho la Urusi: nyekundu nyeusi.

Maana ya Siberia hariri

Kuna namna mbalimbali ya kutaja mipaka ya "Siberia".

Mipaka ya Siberia ya kijiografia ni safu ya milima ya Ural upande wa magharibi, bahari ya Aktika kwa kaskazini, Pasifiki katika Mashariki na nchi za Kazakhstan, Mongolia na Uchina upande wa kusini.

Wakazi hariri

Idadi ya wakazi ni ndogo: kuna milioni 23 pekee. Walio wengi ni Warusi (79%) wanaoishi mjini. Wakazi asilia (21%) ni vikundi vingi vidogo; walio wengi ni wasemaji wa lugha za Kiturki. Utamaduni wao ulikuwa uwindaji na ufugaji lakini sasa ni wachache tu wanaoendelea hivyo.

Hali ya hewa hariri

Hali ya hewa ya Siberia ni kali sana. Kipindi cha joto kina joto kali hadi +40 °C, lakini kipindi cha baridi halijoto hushuka chini hadi -67 °C. Kijiji cha Oymyakon (katika jamhuri ya Sakha) ni mahali baridi duniani; -71.2 °C zilipimwa hapa.

Kipindi cha baridi ni kirefu, kipindi cha joto ni kifupi. Sehemu kubwa ya Siberia inafunikwa na theluji kwa muda wa miezi tisa kila mwaka. Hivyo kilimo kinawezekana katika kanda nyembamba la kusini. Sehemu kubwa nchi imefunikwa na misitu. Lakini maeneo baridi sana ya kaskazini hapana miti tena, ni manyasi na majani tu.

Mito na maziwa hariri

Siberia ina mito mingi mikubwa. Lakini huganda kabisa wakati wa baridi, yaani kwa sehemu kubwa wa mwaka isipokuwa ile katika kusini.

Milima hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Siberia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.