Open main menu
Jozi ya viatu
Jozi ya bata

Jozi ni namna ya kutaja vitu viwili vilivyo pamoja na vinavyofanana. Ni namna nyingine ya kusema "mbili" lakini kwa kukazia tabia ya kuwa pamoja.

Neno latokana na Kiarabu جوزاء jawza inayomaanisha pia "mapacha".

Mifano ya jozi za kawaida ni viatu, soksi, macho. Khanga zinauzwa mara nyingi kwa jozi.