Maporomoko ya maji
Kwa matumizi mengine ya jina angalia maporomoko
Maporomoko ya maji ni mahali ambako maji yanatelemka juu ya kona kwenye mtelemko na kuelekea chini. Kwa kawaida ni sehemu ya njia ya mto au kijito pale ambako maji yanatelemka juu ya ukingo wa mwamba. Lakini inaweza kutokea pia kwenye ukingo wa barafuto pale ambako maji ya myeyuko yanatelemka.
Kutokea na kubadilika kwa maporomoko ya maji
haririMaporomoko ya maji hutokea kwa kawaida katika sehemu za juu ya njia ya mto.[1] Hapa mtelemko kwa jumla ni mkubwa zaidi na mwendo wa maji haraka zaidi. Kwa hiyo nguvu ya maji ni kubwa zaidi kiasi inaweza kuchimba lalio hadi imekuwa mfereji kama korongo mrefu.
Pale ambako mwendo wa maji ni juu ya mwamba mgumu mmomonyoko hutokea polepole tu. Pale yanapofikia mahali ambako mwamba mgumu wa juu unakwisha nguvu ya maji yakitelemka kwenye ukingo inachimba lalio ya chini. Chini ya ukingo hutokea dimbwi yenye kizingia cha maji. Maji yanayozunguko humo pamoja na mawe na mchanga ndani yake yanasuguana kwenye ukuta wa mwamba. Kwa njia upeno au nusu pango hutokea. Kama kuna mwamba laini chini ya takaba ya mwamba mgumu wa juu upanuzi wa pango unaendelea haraka zaidi. Baada ya muda upeno unakatika na kuanguka.[2]
Kwa njia hii ukingo wa maporomoko unarudi nyuma na kurudisha njia ya korongo nyuma. Kasi ya harakati inategemea na tabia za mwamba unaopatikana. Kuna maporomoko yanayorudi nyuma mita na nusu kila mwaka.[3]
Baada ya muda wa kutosha (wakati mwingine miaka mamillioni) nguvu ya maji umeondoa mwamba wa kutosha hali hakuna maporomoko tena na ngazi katika njia imekuwa mtelemko tu.
Picha
hariri-
-
Maporomoko ya Boti, Ghana
-
Maporomoko yanatelemka kwenye Atlantiki (Madeira, Hispania)
-
Black Waterfalls, West Virginia
-
Purakaunui Falls, Newzealand
-
Maporomoko ya Kreealmwasserfall, Austria
Tanbihi
hariri- ↑ Carreck, Rosalind, ed. (1982). The Family Encyclopedia of Natural History. The Hamlyn Publishing Group. pp. 246–248. ISBN 0711202257.
- ↑ "How waterfalls work". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-09-21. Iliwekwa mnamo 2015-05-18.
- ↑ "Observe river erosion creating waterfalls and chasms". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-17. Iliwekwa mnamo 2015-05-18.