West Virginia
West Virginia (Virginia Magharibi) ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika mashariki ya Marekani bara. Imepakana na Ohio, Kentucky, Maryland na Virginia.
West Virginia | |||
| |||
Nchi | Marekani | ||
---|---|---|---|
Mji mkuu | Charleston | ||
Eneo | |||
- Jumla | 62,755 km² | ||
- Kavu | 62,361 km² | ||
- Maji | 394 km² | ||
Tovuti: http://wv.gov/ |
Mji mkuu pia mji mkubwa ni Charleston. Jimbo lina wakazi 1,808,344 (2000) wanaokalia eneo la kilomita za mraba 62,0809.
Kabla ya 1863 eneo la jimbo lilikuwa sehemu za Virginia. Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani Virginia iliondoka katika maungano ya madola ya Marekani ikajiunga na waasi wengine katika Shirikisho la Marekani. Wakati ule wilaya za magharibi ya jimbo zilijitenga na kuwa jimbo jipya lililobaki upande wa maungano. Wilaya hizi ziliendelea kama jimbo la pekee la "West Virginia" hata baada ya mwisho wa vita.
Majimbo ya Marekani |
---|
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu West Virginia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |