Maprotilini (Maprotiline), inayouzwa chini ya jina la chapa Ludiomil miongoni mwa zingine, ni dawa inayotumika kutibu mfadhaiko, wasiwasi, na ugonjwa wa kubadilika-badilika hisia (bipolar disorder).[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kinywa kavu, kuvimbiwa choo, kuhisi usingizi, kizunguzungu na wasiwasi. [1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kujiua, upele, kifafa, kubadilika-badilika hisia, na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida (arrhythmias).[1] Wakati hakuna madhara yake ya wazi kutoka kwetu wakati wa ujauzito, matumizi hayo hayajafanyiwa utafiti vizuri.[2] Dawa hii ni dawa zinazotumika kutibu ugonjwa wa hali ya unyogovu mkubwa (tetracyclic antidepressant (TeCA)). [1]

Maprotilini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1980.[1] Nchini Marekani, vidonge 100 vya miligramu 75 hugharimu takriban dola 175 za Kimarekanai kufikia 2021.[3] Inapatikana katika nchi mbalimbali duniani kote.[4]

Marejeleo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Maprotiline Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Maprotiline (Ludiomil) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Maprotiline Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Index Nominum 2000: International Drug Directory. Taylor & Francis. 2000. ku. 630–. ISBN 978-3-88763-075-1.