Unyogovu (kwa Kiingereza: "Depression") ni hali ya mhemko wa binadamu kuwa chini kiasi cha kumfanya asiweze kujihusisha na shughuli.

Picha hii ya mama mhamiaji imetumika kuonyesha kukata tamaa kwa mwanamke anayejaribu kuilisha familia yake wakati mgumu wa kiuchumi.
Kwenye kizingiti cha ahera, mchoro wa Vincent van Gogh.

Watu wenye hali hii hujisikia na huzuni, wasiwasi, utupu, kukosa matumaini, kuwa wanyonge, wasio na maana, kuhukumika, kuudhika haraka au kuhangaika. Wanaweza kupoteza maslahi katika shughuli ambazo hapo awali ziliwaridhisha, kupoteza hamu ya kula au kinyume chake kula kupindukia, au kuwa na matatizo katika kuzingatia, kukumbuka maelezo au kufanya maamuzi, na wanaweza kutafakari au kujaribu kujiua. Pia kukosa usingizi, kuamka mapema, kulala kupindukia, uchovu, upungufu wa nishati, au kuumwa, maumivu au matatizo ya utumbo yaliyo sugu kwa tiba[1].

Maradhi yenye unyogovu

hariri

Kuna baadhi ya maradhi ya akili yenye unyogovu kama dalili kuu.

Kati ya hayo ni unyogovu mkuu ambayo ni hali ya mtu kupatwa na unyogovu mkuu wa mhemko kwa mara mbili au zaidi akiwa na hali ya huzuni kubwa kama dalili kuu.

Unyogovu sugu (kwa Kiingereza: Dysthymia) ni hali ya huzuni sugu ambayo haina makali ya kufikia kigezo cha unyogovu mkuu wa mhemko. Watu walio na hali ya hisia kinzani (bipolar) wanaweza pia kupatwa na unyogovu mkuu.

Mbali ya matatizo ya unyogovu, unyogovu sugu wa mhemko ni dalili ya tatizo la nafsi la kutohusiana vyema na watu wengine (kwa Kiingereza: Borderline personality disorder).

Ugonjwa wa kurekebishwa akili (kwa Kiingereza: Adjustment disorder) ukiambatana na hisia ya kukata tamaa au unyogovu hutokea kama usumbufu wa kisaikolojia unaotokana na tukio linalotambulika au jambo linaloleta dhiki, ambapo husababisha dalili za mhemko au tabia ambazo ni muhimu lakini hazifikii vigezo vinavyohitajika ili kutambulika kama unyogovu mkubwa wa mhemko. [2]

Jinsi inavyotokea

hariri

Unyogovu unahusishwa na mabadiliko katika dutu katika ubongo (neurotransmitters) ambazo husaidia seli za neva kuwasiliana, kama vile serotonin, dopamine na norepinephrine. Viwango vya dutu hizi zinaweza kuathiriwa na jenetikia, mabadiliko ya homoni, athari za dawa, uzee, majeraha ya ubongo, msimu, na maradhi mengineyo.

Tathmini

hariri

Historia kamili ya hali ya afya, tathmini ya kimwili, na tathmini ya dalili husaidia kutambua sababu ya unyogovu.

Maswali yaliyowiana yanaweza kusaidia kama vile Hamilton Rating scale for depression,[3] na Beck depression inventory.[4]

Kwa ujumla daktari hufanya ukaguzi wa matibabu na uchunguzi au vipimo ili kubaini kama kuna sababu nyingine ya dalili. Vipimo hivi vitajumulisha vipimo vya homoni za kikoromeo (k.m. TSH na thyroxine) ili kuthibitisha mgonjwa hana tatizo la upungufu wa utoaji wa homoni za kikoromeo (hypothyroidism); vipimo vya elektrolaiti na viwango vya kalsiamu katika majimaji ya damu ili kubainisha kuwa mgonjwa hana matatizo ya umetaboli} na hesabu kamili ya chembe za damu ikiwa ni pamoja na ESR ili kuondolea mbali uwezekano wa maradhi ya kuambukiza au maradhi sugu. Ni bora pia kuthibitisha hakuna uwezekano wa madhara ya madawa au pombe. Viwango vya testosteroni vinastahili kubainishwa kuondolea mbali uwezekano wa kupungua kwa nguvu za kiume, ambayo husababisha unyogovu kwa wanaume.[5]

Dalili ya kutoelewa na kutotambua mambo huonekana katika wazee wenye unyogofu lakini inaweza pia kuwa dalili ya mwanzo ya maradhi ya akili yanayoletwa na umri mkubwa (dementing disorder), kama vile ugonjwa wa Alzheimers.[6] [7]

Vipimo vya kuelewa au kutambua mambo na picha za ubongo zinaweza kusaidia kutofautisha unyogovu na shida ya akili.[8]

Michoro kwa mwali elektroniki (CT Scan) inaweza kubainisha maradhi ya ubongo yanayotokea kwa ghafla, au dalili nyingine zisizo za kawaida.[9]

Haimlazimu daktari kufanya uchunguzi wa ujumla tena maradhi yanapochipuka tena kama hakuna sababu maalum ya kiafya.

Marejeo

hariri
  1. "Depression". National Institute of Mental Health. 2009-09-23. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-11. Iliwekwa mnamo 2010-05-22.
  2. American Psychiatric Association 2000a, p. 355
  3. Zimmerman M, Chelminski I, Posternak M (2004 Sep). "A review of studies of the Hamilton depression rating scale in healthy controls: implications for the definition of remission in treatment studies of depression". J Nerv Ment Dis. 192 (9): 595–601. PMID 15348975. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  4. McPherson A, Martin CR (2010 Feb). "A narrative review of the Beck Depression Inventory (BDI) and implications for its use in an alcohol-dependent population". J Psychiatr Ment Health Nurs. 17 (1): 19–30. PMID 20100303. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  5. Orengo C, Fullerton G, Tan R. Male depression: A review of gender concerns and testosterone therapy. Geriatrics. 2004;59(10):24–30. PMID 15508552.
  6. Reid LM, Maclullich AM. Subjective memory complaints and cognitive impairment in older people. Dementia and geriatric cognitive disorders. 2006;22(5–6):471–85. doi:10.1159/000096295. PMID 17047326.
  7. Katz IR. Diagnosis and treatment of depression in patients with Alzheimer's disease and other dementias. The Journal of clinical psychiatry. 1998;59 Suppl 9:38–44. PMID 9720486.
  8. Wright SL, Persad C. Distinguishing between depression and dementia in older persons: Neuropsychological and neuropathological correlates. Journal of geriatric psychiatry and neurology. 2007;20(4):189–98. doi:10.1177/0891988707308801. PMID 18004006.
  9. Sadock 2002, p. 108