Marc Batchelor

Mchezaji wa chama cha soka cha kitaaluma na mtangazaji kutoka Afrika Kusini (1970-2019)

Marc Batchelor (4 Januari 1970 - 15 Julai 2019) alikuwa mchezaji wa soka wa Afrika Kusini ambaye alicheza kama mshambuliaji.

Maisha na kazi

hariri

Batchelor alijiunga na timu mbalimbali nchini Afrika kusini ikiwemo Wanderers, Balfour Park, Berea Park, Defence na Dynamos mwaka 1990.[1][2] Baadaye alicheza katika klabu ya Bidvest Wits F.C, Orlando Pirates, SuperSport United, Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns na Moroka Swallows. Alishinda mataji manne makubwa akiwa na klabu ya Orlando Pirates ikijumuisha Kombe la Mabingwa wa Afrika la mwaka 1995.[3] Baada ya kustaafu kwenye soka la kulipwa mwaka 2003 alifanya kazi kama mchambuzi wa mpira wa televisheni. Hata hivyo, alifutwa kazi mwaka 2007 baada ya kupigana katika mgahawa Mwaka 2014 Batchelor alikuwa shahidi katika kesi ya Oscar Pistorius.[4] Aliuwawa nje ya nyumbani kwake huko Olivedale tarehe 15 Julai 2019.[1][3][5][6]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "Marc Batchelor - Soweto Derby legend | Goal.com". www.goal.com.
  2. "'Man-mountain of a striker' was larger than life". The Citizen (Gauteng).
  3. 3.0 3.1 "Tributes pour in for slain ex-footballer Marc Batchelor". Sport. 16 Julai 2019.
  4. Culpepper, Chuck (10 Machi 2014). "A key witness may address Oscar Pistorius and fidelity". sportsonearth.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-16. Iliwekwa mnamo 28 Agosti 2019. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  5. "Marc Batchelor: South African former footballer shot dead". BBC Sport. 16 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 28 Agosti 2019.
  6. Ratsie, Ofentse. "Orlando Pirates mourns their former player Marc Batchelor". TimesLIVE. Iliwekwa mnamo 28 Agosti 2019.
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marc Batchelor kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.