Margaret Karembu
Margaret Gathoni Karembu ni mwalimu wa sayansi na mtaalamu wa usimamizi wa sayansi wa nchini Kenya mwenye ujuzi katika nyanja za uhamishaji wa teknolojia na matumizi ya bioteknolojia barani Afrika. Pia ni Mkurugenzi wa ISAAA, shirika la kimataifa lisilo la faida linaloshiriki bioteknolojia ya kilimo kwa kujihusisha na uhandisi wa vinasaba. Pia, ni mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Mpango wa Majadiliano ya Wazi kuhusu Bioteknolojia ya Kilimo, Tawi la Kenya.[1]
Majukumu yake katika ISAAA yanajumuisha kupanga na kusimamia vipengele vyote vya programu za AfriCenter ambazo zinajumuisha uhamishaji wa bioteknolojia za kilimo kati ya nchi zilizoimarishwa na nchi zinazoendelea. Yeye pia anashiriki katika kusambaza taarifa kuhusu bioteknolojia ya kisasa ya kilimo ili kuhamasisha maamuzi yenye ufahamu kuhusu masuala yenye mvutano kama vile GMO.[2]
Awali alitumikia kama Mwenyekiti wa Baraza na Makamu Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Ushirika cha Kenya baada ya hapo alitumikia Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Meru. [2]
Mnamo mwezi Desemba 2000,mradi wake uliohusisha kutathmini na kuhamisha teknolojia ya upandaji wa ndizi kwa kutumia mbinu ya tishu , ulishinda Medali ya Kwanza ya Utafiti katika tuzo za Global Development Network (GDN) kwa 'Sayansi na Teknolojia kwa Maendeleo' zilizofadhiliwa na Serikali ya Japani na Benki ya Dunia.[3]
Elimu na Kazi.
haririKuanzia mwaka wa 1992 hadi 2002, Karembu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, nchini Kenya.[1] Wakati huu, alipata uzoefu mkubwa kwenye masuala ya utafiti wa usambazaji wa teknolojia katika kilimo kidogo. Mnamo mwaka wa 2000, mradi wake uliohusisha kutathmini na kuhamisha teknolojia ya upandaji wa ndizi kwa kutumia mbinu ya tishu kwa kuwanufaisha zaidi ya wakulima 5,000 barani Afrika Mashariki, Mradi huu ulitunukiwa Medali ya Kwanza ya Utafiti katika tuzo za Global Development Network (GDN) kwa 'Sayansi na Teknolojia kwa Maendeleo' zilizofadhiliwa na Serikali ya Japani na Benki ya Dunia.
Mnamo mwaka wa 2002, alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Elimu ya Sayansi ya Mazingira na tasnifu yake ilihusu: "Mchango wa Shule za Msingi katika Kuboresha Mazingira Nchini Kenya. Kesi ya Wilaya ya Kiambu.". Mwaka wa 2003, alijiunga na ISAAA[1]
Mnamo mwaka wa 2008, alikamilisha Kozi ya Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika Shule ya Utawala ya Kennedy, Chuo Kikuu cha Harvard. Mnamo mwaka wa 2011, alihudhuria Kozi ya Uongozi wa Kimkakati na Usimamizi wa Mabadiliko kwa Wakurugenzi wa Mashirika ya Serikali katika Taasisi ya Usimamizi ya Kenya na Kozi ya Uongozi ya USAID's Champions for Change. Mnamo mwaka wa 2015, alihudhuria Kozi ya Uongozi wa Bayoteknolojia katika Muungano wa Sayansi wa Chuo Kikuu cha Cornell.[2]
Anaratibu Vituo vya Habari vya Bayoteknolojia vya ISAAA barani Afrika ambavyo vinatoa taarifa kwa Kiingereza, Kiswahili na Kifaransa.[1]
Uanaharakati
haririKarembu amekuwa mhamasishaji wa muda mrefu wa bioteknolojia. Mnamo mwaka wa 2001, kama mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kenyatta, alihojiwa na jarida la New Scientist kuhusu propaganda kutoka kwa baadhi ya mashirika ya kijani barani Ulaya kuhusu bayoteknolojia, ambayo imezuia juhudi za kupambana na njaa barani Afrika. Katika mahojiano hayo, Karembu alisema, "Hatupati data, tunapata maoni."[4]
Mnamo mwaka wa 2014, aliandika makala ya maoni kwa ajili ya Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Chakula ya Kimataifa iliyochapishwa kwenye SciDev.net yenye kichwa: "Matatizo na Hoja Dhidi ya Mazao ya GM" ambapo alionyesha kuwa kufikia mwaka wa 2013, zaidi ya wakulima milioni 18 (ambao angalau asilimia 90 walikuwa wakulima wadogo wenye rasilimali chache katika nchi zinazoendelea) walikuwa wamechagua kutumia mazao yaliyobadilishwa vinasaba kwenye zaidi ya hekta milioni 175 za ardhi ya kilimo. "Ushahidi mpya unaonyesha kuwa hoja dhidi ya mazao ya GM hazina msingi," alisema Margaret Karembu. "Kinyume na maoni yanayoshikiliwa sana kwamba teknolojia ya GM itawanufaisha tu mashirika makubwa na inakusudiwa kwa wakulima wakubwa, mwenendo wa hivi karibuni unaonyesha vinginevyo.[5][6]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 https://africenter.isaaa.org/team/margaret-karembu/
- ↑ 2.0 2.1 2.2 https://foodinsight.org/wp-content/uploads/2015/04/Margaret-Karembu.pdf
- ↑ "Kenyan Researchers". kenyayearbook.co.ke. 2011. Retrieved 7 November 2019.
- ↑ Coghlan, Andy. "Green menace". New Scientist. 170 (2297). Retrieved 2020-04-02
- ↑ Karembu, Margaret (6 March 2014). "The problems with the arguments against GM crops". SciDev.net. Retrieved 7 November 2019.
- ↑ Dr Margaret Karembu: The state of play for GM crops in Africa on YouTube
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Margaret Karembu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |