Margaret Jean Roberts Legum (8 Oktoba 1933, Pretoria, Afrika Kusini - 1 Novemba 2007, Cape Town, Afrika Kusini) alikuwa mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi na marekebisho ya kijamii kutoka Afrika Kusini na Uingereza, ambaye alijikita katika uchumi.

Legum alihudhuria Chuo Kikuu cha Rhodes na Newnham College ambapo alisomea uchumi. Alifunga ndoa na Colin Legum mnamo 1960 na wakaenda kuishi London.[1]

Margaret Legum alifariki dunia mnamo mwaka wa 2007, akiwa na umri wa miaka 74, kutokana na saratani, akiacha nyuma binti zake watatu na wajukuu.[2]

Legum alikuwa mwanzilishi wa Mtandao wa Uchumi Mpya wa Afrika Kusini.[3] Kitabu chake, "It Doesn't Have To Be Like This: Global Economics - A New Way Forward" (2003), kilichoandikwa kwa msingi wa mfululizo wa mihadhara aliyotoa katika Chuo Kikuu cha Cape Town.[4]

Alifahamika sana kwa kitabu chake cha mwaka wa 1963 kinachohusu umuhimu wa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Afrika Kusini, "South Africa: Crisis for the West", ambacho aliandika pamoja na mumewe, Colin.[5]

Marejeo

hariri
  1. Herbstein, Denis (2007-11-16), "Margaret Legum", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2024-05-14
  2. "Journalist Margaret Legum passes away". The Mail & Guardian (kwa Kiingereza). 2007-11-02. Iliwekwa mnamo 2024-05-14.
  3. "Dictionary of National Biography", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-03-01, iliwekwa mnamo 2024-05-14
  4. http://peacenews.info/node/5001/margaret-legum-it-doesnt-have-be-global-economics-new-way-forward
  5. http://www.scotsman.com/news/obituaries/margaret-legum-1-698625
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Margaret Legum kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.