Marie-Rose Nizigiyimana

Marie-Rose Nizigiyimana (alizaliwa mnamo mwaka 1966) ni Mwanasiasa wa Burundi. Aliwahi kushika nyadhifa ya Uwaziri wa Biashara, Viwanda na utalii katika serikali ya Rais Pierre Nkurunziza kuanzia tarehe 18 Februali mpaka alipofukuzwa kazi 18 Mei 2015.[1]

Biografia

hariri

Nizigiyimana alizaliwa mnamo mwaka 1966 katika jamii ya Rango huko jimbo la Kayanza. [2] Alipata elimu yake ya shahada yake ya kwanza ya Ualimu mwaka 1993. Nizigiyimana alikua mwanasiasa wa chama cha Union for National Progress tangu mwaka 1993. 18 Februali 2014 alichaguliwa kuwa Waziri wa Biashara, Viwanda na utalii baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri.[3]

Alifukuzwa uwaziri 18 Mei 2015, baada ya kushindwa kwa majaribio ya mapinduzi ya kijeshi.[4] Hii ni baada ya ukosoaji mkubwa juu ya upungufu wa mafuta nchini Burundi. Nafasi yake ilichukuliwa na Irina Inantore.[5]

Marejeo

hariri
  1. https://web.archive.org/web/20150520221421/http://www.punchng.com/news/burundi-president-reshuffles-cabinet/
  2. Nadine Nkengurutse (24 February 2014). "Marie-Rose Nizigiyimana : le Commerce dans les mains d'une licenciée en Histoire" (in French). iwacu. Archived from the original on 20 May 2015. Retrieved 19 May 2015.
  3. "Burundi President reshuffles cabinet". Punch. 18 February 2014. Archived from the original on 20 May 2015. Retrieved 19 May 2015.
  4. http://www.washingtontimes.com/news/2015/may/18/after-coup-attempt-burundi-president-fire-3-minist/
  5. http://www.premiumtimesng.com/foreign/africa/183235-burundian-leader-sacks-defence-minister.html