Marina Barampama

Mwanasiasa wa Burundi.

Marina Barampama (aliyezaliwa mwaka 1969) ni mwanasiasa wa Burundi. Alichaguliwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais tarehe 8 Septemba 2006, akichukua nafasi ya Alice Nzomukunda. Alikaa kwenye wadhifa huo kwa muda wa miezi sita, hadi alipofutwa kazi kwa kosa la kumuunga mkono Hussein Radjabu. Aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Kitaifa la Kulinda Demokrasia-Vikosi vya Kulinda Demokrasia (CNDD–FDD), sasa ni Katibu Mkuu wa Muungano wa Amani na Maendeleo.[1]

Kazi zake za Kisiasa hariri

Baada ya kujiuzulu kwa Makamu wa Rais Alice Nzomukunda kutokana na ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu, Barampama aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais Pierre Nkurunziza tarehe 8 Septemba mnamo mwaka 2006. Alikuwa miongoni mwa wanachama kujulikana sana kutoka chama cha upinzani cha Union for National Progress (UPRONA) , alitolewa ya kura ya upinzani kupinga habari potofu zilizotolewa kumhusu. Baadaye walibishana kwamba uchaguzi wa Barampama haukuwa halali, kwani bila wanachama wao, hapakuwa na wanachama wa kutosha waliopiga kura kuunda akidi hiyo.[2]

Alifutwa kazi na Nkurunziza tarehe 8 Februari mnamo mwaka wa 2007, alihusishwa na makosa ya ukaidi na kutowajibika ipasavyo. Barampama alikuwa mfuasi wa Hussein Radjabu ambaye alikuwa mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Kitaifa la Kutetea Demokrasia - Vikosi vya Kulinda Demokrasia (CNDD-FDD), ambaye naye alifukuzwa akiwa na wadhifa wa mwenyekiti na Rais muda mfupi kabla ya kutimuliwa kwa Barampama.[3] Radjabu baadaye alikamatwa na kufungwa jela kwa muda wa miaka 13 kwa kosa la uasi.[4]

Baadaye alibadili utii wake kwa Umoja wa Amani na Maendeleo (UPD) na kufikia mwaka 2015 akawa Katibu Mkuu wa chama hicho. Kufuatia ongezeko la ghasia zilizoonekana katika machafuko ya Burundi na baada ya mauaji ya msemaji wa chama Patrice Gahungu, Barampama alihofia maisha yake kwani alisema kuwa UPN ilionekana kuwa tishio kwa serikali.[5]

Marejeo hariri

  1. "'Kila siku tunataka kurudi Burundi lakini nafasi haijapatikana'". BBC News Swahili (kwa Kiswahili). 2020-06-11. Iliwekwa mnamo 2022-03-18. 
  2. 'Unknown' elected as Burundi VP (kwa en-GB), 2006-09-08, iliwekwa mnamo 2022-03-18 
  3. Burundi's president sacks deputy (kwa en-GB), 2007-02-09, iliwekwa mnamo 2022-03-18 
  4. Burundi jail term for 'plotter' (kwa en-GB), 2008-04-04, iliwekwa mnamo 2022-03-18 
  5. "Burundi: le porte-parole d’un parti d’opposition tué à Bujumbura". RFI (kwa Kifaransa). 2015-09-08. Iliwekwa mnamo 2022-03-18. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marina Barampama kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.