"Marry You" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 2 Februari, 2017 kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz akimshirikisha Ne-Yo kutoka nchini Marekani. Wimbo unatoka katika albamu ya A Boy From Tandale na wa nne kutolewa kama single kutoka katika albamu hiyo. Wimbo umetayarishwa na Sheddy Clever wa Burn Records. Kitendo cha Diamoand kufanya ngoma na msanii mkubwa kama Ne-Yo kilishangaza ulimwengu wa muziki wa Bongo Flava kupita kiasi. Hata wazo la kutoa albamu ikiwa na wasanii wazito ilianza tangu 2016 au nyuma zaidi.[1]

“Marry You”
“Marry You” cover
Kava ya Marry You
Single ya Diamond Platnumz na Ne-Yo
kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale
Imetolewa 2 Februari, 2017
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2016
Aina Bongo Flava, Afro-pop, R&B
Urefu 4:08
Studio Burn Records
Mtunzi Diamond Platnumz
Ne-Yo
Mtayarishaji Sheddy Clever
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz na Ne-Yo
"Salome"
"(2016)"
"Marry You"
"(2017)"
"I Miss You"
(2017)

Pamoja na kutayarishwa na Sheddy, lakini kazi ya utayarishaji ilifanyika nchini Kenya. Studio haijulikani, lakini picha za video za awali zilifanyiwa nchini humo kabla kwenda kumaliziwa mazima huko nchini Afrika Kusini na baadaye Marekani. Wimbo una mandhari mengi ya kutumika katika harusi. Isitoshe, hii ilikuwa ndoto ya miaka mingi ya Diamond kufanya kazi na msanii anayempenda kutoka moyoni mwaka Ne-Yo. Katika kushirikiana, imekuwa kama ndoto imetimia vile.[2]

Vilvile wimbo umetolewa katika akaunti tofauti na ile ambayo Chibu huitumia kusambazia video zake. Hii ilienda katika akaunti yake mpya ya YouTube iliyoitwa DiamondVevo badala ya ile ya "Diamond Platnumz". Halafu ndio wimbo wa kwanza kusambazwa na "Universal Music" ya Afrika Kusini na kushinda platinamu sita katika nyimbo zilizopakuliwa sana kupitia iTune kwa nchini humo.[3][4][5] Na ndiye msanii wa kwanza wa Afrika kuingia nao mkataba na msanii wa kwanza Afrika kufikisha mauzo yenye platinamu 6.[6]

Tazama pia hariri

Marejeo hariri