Mary Deo Muro ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CHADEMA. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti maalum vya wanawake kwa miaka 20152020. [1] Amehitimu shahada katika Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) [1]

Kabla ya kuingia Bungeni aliwahi kutumikia nafasi mbalimbali ndani ya CHADEMA ikiwemo Mwenyekiti wa vuguvugu la CHADEMA ni msingi Mkoa wa Pwani mnamo 2015. Mnamo 2009 alichaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho jimbo la Kibaha Mjini kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) ndani ya jimbo hilo nafasi aliyoitumikia mpaka 2015.

Mnamo 2020 alitangaza kugombea nafasi ya Ubunge jimbo la Kibaha mjini lakini hakufanikiwa kuipeperusha bendera ya chama hicho baada ya kushindwa katika kura za maoni dhidi ya Michael Mtaly.

Mary kwa sasa ni Katibu wa BAWACHA Mkoa wa Pwani Kaskazini akijihusisha pia na biashara na kilimo cha mazao ya biashara.

Marejeo

hariri
  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017

2.http://parliament.go.tz/polis/members/326