Mary Spio
Mary Spio ni mhandisi wa anga za juu, mvumbuzi wa teknolojia na mjasiriamali. Ndiye Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa CEEK Virtual Reality. [1] [2] [3]
Mary Spio | |
---|---|
| |
Nchi | Ghana |
Kazi yake | Mwandisi wa anga |
Maisha ya mapema na elimu
haririSpio alilelewa Ghana. Alisomea elimu yake ya sekondari Shule ya Upili ya Holy Child huko Cape Coast. [4] Akiwa na umri wa miaka 16 alihamia kukaa Syracuse, New York nchini Marekani. Alisoma Chuo Kikuu cha Syracuse, na kuhitimu Shahada ya Sayansi ya uhandisi wa umeme mnamo 1998. Baadaye alifuata shahada ya uzamili ya uhandisi wa umeme na sayansi ya kompyuta kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Georgia.
Marejeo
hariri- ↑ Adona, Nadia (2017-02-16). "Mary Spio". segd.org (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-18. Iliwekwa mnamo 2021-02-23.
- ↑ Spio, Mary. "Mary Spio". Entrepreneur (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-02-23.
- ↑ "Mary Spio - keynote speaker". Global Speakers Bureau (kwa Kipolandi). Iliwekwa mnamo 2021-02-23.
- ↑ "Mary Spio". F6S (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-02-23.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mary Spio kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |