Masinde muliro (alizaliwa mnamo 1922 na aliaga dunia mnamo 14 Agosti 1992) alikuwa mwanasiasa wa Kenya, mmoja wa viongozi wakuu katika kuchagiza siasa nchini Kenya. Alikuwa mpigania uhuru aliyejulikana na alifanya kampeni kwa ajili ya marejesho ya demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya katika miaka yake ya mwisho. Alikuwa muhawiliki asiye na mzaha wala huruma na mtu wa amani aliyejihusisha sana kwa siasa. Mmoja wa wanasiasa safi zaidi katika historia ya Kenya , rekodi ambayo inaweza pinzaniwa tu na Musikari Kombo na Ronald Ngala. Alikuwa anajulikana kama mmoja wa viongozi bora ambao kamwe hawakuwahi kuwa rais, na kama hangeupa dunia mkono wa buriani, nafasi zilikuwa kwamba angemshinda Daniel Arap Moi kwa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 1992.

Maisha Yake ya Awali hariri

Henry Pius Masinde Muliro alizaliwa katika eneo la Kimilili nchini Kenya, mwana wa Muliro Kisingilie na mkewe Makinia. Wazazi wake walikufa wakati alipokuwa mchanga na alilelewa na kaka wa kambo, Aibu Naburuku. Baada ya masomo ya shule ya msingi na ya upili nchini Kenya na Uganda, alijiunga na Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini mwaka wa 1949. Alijiunga na kozi ya Shahada ya Sanaa katika Kiingereza, Historia na Falsafaya Siasa, na alihitimu mwaka wa 1953 akiwa na shahada za na Sanaa na Elimu. Mwaka wa 1954 alirejea nyumbani na mke wa asili ya Afrika Kusini, na alifundisha kwa muda katika shule ya serikali. Mwaka wa 1957, alipiga moyo konde kuiacha kazi hiyo ya ualimu na kujiunga na siasa.

Siasa hariri

Mwaka wa 1948, Muliro alijiunga na chama cha Kenya African Union (KAU), chama kilichoanzishwa kutetea maslahi ya Waafrika nchini Kenya ambayo wakati huo ilikuwa chini ya ukoloni. Alipoacha kufunza mwaka wa 1957, aligombea kiti cha ubunge cha eneo bunge la Nyanza Kaskazini ambacho wakati huo kilikuwa kinashikiliwa na W.W.W. Awori (kakake mkongwe wa makamu wa rais wa zamani wa Kenya, Moody Awori). Muliro alishinda uchaguzi. Miongoni mwa wabunge wenzake walikuwa Daniel Arap Moi ambaye aliyekuwa anawakilisha Bonde la Ufa, Tom Mboya ambaye aliyekuwa anawakilisha eneo la Nairobi, Bernard Mate ambaye aliyekuwa anawakilisha Mkoa wa Kati, Ronald Ngala ambaye aliyekuwa anawakilisha Mkoa wa Pwani, James Nzau Muimi ambaye aliyekuwa anawakilisha Mkoa wa Mashariki, Lawrence Oguda ambaye aliyekuwa anawakilisha Nyanza Kusini na Oginga Odinga ambaye aliyekuwa anawakilisha Nyanza ya Kati. Mwaka wa 1958 Muliro alianzisha chama cha Kenya National Party huku akiungwa mkono na wanachama 9 wa Legco(Legislative Council). Kisha alikibomia chama hicho na kujiunga na chama cha Kenya African Democratic Union (KADU). Hatimaye aliteuliwa kama Waziri wa Biashara kabla tu ya Kenya kupata uhuru mwaka wa 1963. Muliro alihudumu katika nyadhifa mbalimbali katika serikali za baadaye, lakini mara kwa mara alikuwa katika upande mbaya wa Rais Jomo Kenyatta. Baada ya kifo chake Kenyatta, Muliro alirejea Bungeni baada ya kushinda ombi mahakamani. Alihudumu kama mbunge wa eneo bunge la Kitale Mashariki hadi mwaka wa 1988, wakati eneo bunge hili liligawanywa. Alishinda kiti kipya cha ubunge cha eneo bunge la Cherangany mwaka wa 1988, lakini alishikilia nyadhifa hiyo kwa muda wa miaka miwili tu. Katika uchaguzi wa wabunge wa mwaka wa 1990, kiti hicho cha Cherangany kilishindwa na Kipruto Arap Kirwa.

Kampeni ya Vyama vingi hariri

Mwaka wa 1989, Muliro aliungana na Kenneth Matiba, Charles Rubia, Martin Shikuku, Phillip Gachoka na Oginga Odinga kuunda FORD (Forum for Restoration of Democracy), ni kundi shinikizo lililotaka kurejeshwa kwa siasa ya vyama vingi. Baada ya mapigano ya vurugu kati ya wafuasi wa FORD polisi na wafuasi wa serikali na polisi, serikali ya KANU lilikubali siasa ya vyama vingi mwaka wa 1991. FORD ikawa chama huku Muliro akiwa Makamu wa Mwenyekiti.

Kutoelewana kuliepuka kati ya wapinzani wakuu wawili, Oginga Odinga na Kenneth Matiba, kila mmoja wao akigombea urais na kutotaka kuwasikiliza wanachama wenzao. Ilikuwa muda mfupi baadaye wakati Muliro aliondoka na kuelekea London ili kuchangisha fedha kwa ajili ya chama kipya cha kisiasa cha Ford. Ilikuwa safari ya bahati mbaya: kwani alipokuwa anarejea, alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nairobi asubuhi ya tarehe 14 Agosti 1992 akizimia na kufa. Utata wa kifo chake uliimarishwa kwa kutokuwepo kwa uchunguzi rasmi wa mwili yake. Muliro alizikwa katika shamba yake katika eneo la Kitale nchini Kenya.

Chama cha FORD kiligawanyika katika makundi mawili baada ya kifo cha Muliro kutokana na kutokubaliana kuhusu na nani ambaye angegombea kiti cha urais dhidi ya Rais Moi. Kenneth Matiba na Martin Shikuku wakidai kuwa wao ndio wamiliki halisi wa FORD na walijiondia na kuunda chama cha Ford Asili huku Odinga na wengine wakijitenga na kuunda Ford Kenya. . Iwapo Masinde Muliro hangeaga dunia, FORD ya awali ingebakia kwa umoja na pengine chama hiki kingemwondoa rais Moi na chama tawala cha KANU utawalani katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 1992.

Marejeo hariri

  • Simiyu Wandiiba. Masinde muliro: A Biography (Nairobi: EAEP, 1996)