Matema ni kata ya Wilaya ya Kyela katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Matema iko kwenya mwambao wa Ziwa Nyasa, mguuni pa milima ya Livingstone, karibu na ncha ya kaskazini kabisa ya ziwa.

Kata ya Matema
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Kyela
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 12,231
Matema ufukoni

Msimbo wa posta ni 53715.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 12,231 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,103 [2] walioishi humo.

Wakazi wanajushughulisha kwa uvuvi na kilimo.

Matema ni mahali penye utalii kiasi kutokana na wageni wanaotafuta raha ufukoni. Katika mazingira ya Matema ufuko ni wa mchanga tu, kwa hiyo hakuna majani kwenye maji, na kutokana na hali hii hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa kichocho (bilharzia) ni ndogo sana.

Pia Matema ni mahali pekee kwenye ufuko wa Nyasa panapofikiwa kwa barabara na kufaa kwa kuogelea na kupumzika kutoka upande wa Tukuyu na Mbeya. Hata hivyo kilomita za mwisho za barabara zina matatizo, hasa majira ya mvua.

Kuna nyumba za wageni zinazomilikiwa na Dayosisi ya Konde ya Kanisa ya Kiluteri, pia nyingine ya Kanisa la Uinjilisti la Mbalizi na nyingine ya Kanisa Katoliki.

Kuna nyumba ya kihistoria ya wamisionari Walutheri kutoka misioni ya Berlin ambayo leo ni sehemu ya nyumba ya wageni.

Waluteri wana sahanati kubwa na pia chuo cha Biblia.

Tangu mwaka 2010 Matema imeunganishwa kwenye mtandao wa umeme wa TANESCO.

Kila Ijumaa kuna soko la wafinyanzi wanaoleta mitungi yao kutoka kijiji cha Ikombe kilichopo ng'ambo ya ziwa kwenye rasi ya Ikombe wakisafirisha vyombo kwa njia ya mashua.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Kyela DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-12. 
  Kata za Wilaya ya KyelaMkoa wa Mbeya - Tanzania  

Bondeni | Bujonde | Busale | Ibanda | Ikama | Ikimba | Ikolo | Ipande | Ipinda | Ipyana | Itope | Itunge | Kajunjumele | Katumbasongwe | Kyela | Lusungo | Mababu | Makwale | Matema | Mbugani | Mikoroshoni | Muungano | Mwanganyanga | Mwaya | Ndandalo | Ndobo | Ngana | Ngonga | Njisi | Nkokwa | Nkuyu | Serengeti | Talatala


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Matema kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.