Matumbawe
Matumbawe ni wanyama wadogo wa faila Cnidaria ya wanyama-upupu.
Kila mnyama ana umbo la mfuko mwenye urefu wa milimita au sentimita chache; uwazi upande mmoja ni mdomo na pia mkundu unaoviringishwa na minyiri.
Kuna aina nyingi na tofauti za matumbawe lakini kwa jumla hawatembei bali hukaa pamoja chini ya maji ya bahari mahali pamoja. Spishi nyingi za matumbawe hujijengea kiunzi nje wakitumia chokaa kinachopatikana katika maji ya bahari na kujenga ama msingi wa kukaa imara au chumba kidogo cha kujikinga. Wakati tumbawe anakufa wengine huendelea kijenga juu ya viunzi nje vitupu vya watangulizi vyao. Kwa njia mwamba tumbawe unaanza kukua; visiwa vingi vya bahari tropiki vimefanywa na mwamba tumbawe.
Other websites
hariri- Coral Reefs and Hard Grounds information Ilihifadhiwa 1 Februari 2010 kwenye Wayback Machine. from the Florida Fish and Wildlife Conservation Commission Fish and Wildlife Research Institute Ilihifadhiwa 4 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine.
- Coral Reefs of the Tropics Ilihifadhiwa 19 Februari 2011 kwenye Wayback Machine.: facts, photos and movies from The Nature Conservancy
- Australian Coral Records Research Group Ilihifadhiwa 28 Machi 2011 kwenye Wayback Machine.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: