Mnyama-upupu
Mnyama-upupu | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Konyeza sahihi (Chrysaora fuscescens)
| ||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||
| ||||||
Ngazi za chini | ||||||
Nusufaila na ngeli:
|
Wanyama-upupu (kutoka Kiholanzi neteldier) ni wanyama sahili wa bahari au maji baridi ambao wana seli zinazochoma ngozi na zinazoweza kukamata samaki na wanyama wadogo wengine. Anthozoa kama matumbawe wamekazika chini lakini takriban wote wa Medusozoa huogelea majini. Spishi chache kiasi tu zinatokea majini baridi.
Mwili wa wanyama-upupu umeumbwa kwa tabaka la kolajini (collagen) na proteoglycans lililofunikwa na seli nje na ndani. Tabaka la nje la seli liitwa exodermi (exoderm) na tabaka la ndani liitwa gasterodermi (gastroderm). Kati ya mwili ni uwazi wa mmeng'enyo ulio na kipenyo kimoja kilikopo juu katika Anthozao na chini katika Medusozoa. Anthozoa wana minyiri mifupi kiasi kuzunguka kipenyo hiki, lakini minyiri ya konyeza ni mirefu.
Picha
hariri-
Wanyama-marija
-
Spishi mbalimbali za wanyama-marija (na kiti cha pweza)
-
Ua-bahari njano
-
Ua-bahari kijani
-
Maua-bahari machungwa
-
Konyeza-sanduku
-
Hidra
-
Yavuyavu
-
Konyeza-masikio
-
Konyeza madoa
-
Konyeza-kikonyo
-
Konyeza-kikonyo juu ya nyasi-bahari
-
Kidusia cha kalambezi (Myxozoa)
-
Polypodium hydriforme