Mbio za Langalanga

michuano ya motorsport iliyofanyika duniani kote

Mbio za Langalanga, maarufu kwa jina la Kiingereza Formula 1 au F1, ni mashindano ya juu kabisa katika kitengo cha mashindano ya magari yenye uwazi ya siti moja inayosimamiwa na Shirika la mashindano ya magari (FIA). Mashindano ya Mbio za Langalanga yamekua mashindano yaliyorushwa kwenye matangazo zaidi ya mashindano mengine yoyote ya magari tangu yalipoanzishwa mwaka 1950. Katika lugha ya Kiingereza, neno Formula Racing humaanisha sheria na taratibu zinaatotakiwa kuzingatiwa kwenye kila gari la mshiriki wa mashindano. Msimu wa Mbio za Langalanga huusisha mfululizo wa mashindano unaofahamika kwa jina la Grands Prix. Grands Prix hufanyika katika nchi na mabara tofauti katika barabara maalum au barabara za uma zilizofungwa. Mfumo maalumu wa kuhesabu alama unatumika kwenye Grands Prix ili kupata washindi wawili wa msimu: Msindi katika kitengo cha dereva na mshini katika kitengo cha magari (timu). Kila dereva mshiriki lazima awe na leseni ya FIA Super Licence, hii ni leseni ya juu kabisa katika kitengo cha leseni za mashindano inayotolewa na FIA, na mashindano lazima yafanyike katika barabara maalumu zilizoidhinishwa na FIA kulingana na matakwa na sheria elekezi.

Magari ya Mbio za Langalanga ndio magari ya kasi zaidi katika kitengo cha Magari ya mashindano, yana uwezo wa kuzunguka kona kwa kasi ya juu sana kwa kutengeneza mgandamizo wa hewa, mgandamizo huu hutengengenezwa na muundo wa mbele wa gari wenye mabawa maalumu. Magari hayo hutegemea zaidi vifaa vya umeme, mfumo wa kukata upepo, Suspension na matairi maalumu. Mifumo ya kuzuia gari kuteleza, kusukuma kwari kwa kasi wakati wa kuanza, gia za automatiki na mifumo mingine inayomsaidia dereva wakati wa mashindano vilipigwa marufuku kwa mara ya kwanza mwaka 1994. Mifumo hii ilirudishwa tena kwa kiasi kidogo mwaka 2001, lakini vilipigwa marufuku kwa mara nyingine mwaka 2004 na 2008.[1]

Ikiwa wastani wa garama za kuendesha timu – kubuni, kujenga na kuboresha magari, mishahara, usafiri kwa kukadiria inafika £220,000,000 (au $265,000,000),[2] Vita vingi vya kifedha na kisiasa vimeripotiwa. Formula One Group inamilikiwa na Liberty Media, iliinunua mwaka 2017 kutoka kwenye kampuni binafsi CVC Capital Partners kwa kiasi cha £6.4 bilioni ($8 bilioni).[3][4]

Tanbihi

hariri
  1. "F1 bans traction control for 2008", BBC Sport, 30 March 2007. 
  2. Sylt, Christian. "Formula One budget cuts are expected to crash 1,600 jobs", 20 April 2020. (en) 
  3. "Bernie Ecclestone removed as Liberty Media completes $8bn takeover", 23 January 2017. "Bernie Ecclestone has been removed from his position running Formula 1 as US giant Liberty Media completed its $8bn (£6.4bn) takeover of the sport." 
  4. "Liberty Media Corporation Completes Acquisition of Formula 1". Liberty Media Corporation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Desemba 2019. Iliwekwa mnamo 7 Desemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri