Mbute ni chakula kinachotokana na zao la muhogo ambao humenywa na kuvundikwa kwa maji halafu huchemshwa.

Chakula hicho huwa kitamu kupita muhogo uliopikwa.

Maandalizi ya mbute

hariri

Mbute hutokana na zao la muhogo ambapo humenywa na kuanikwa kwa muda halafu huvunda kwa muda. Baadaye huchukuliwa na kupikwa hadi huwa tayari kuliwa.mbute huweza kuliwa kama chakula cha asubuhi, mchana pia hata jioni chakula hiki huweza kutumiwa na watu wa lika lote wakiwemo watoto, vijana pamoja na wazee.

Matumizi ya mbute

hariri

Mbute hutumika kwa ajili ya chakula kwa mwanadamu hususani katika jamii za kiafrika kama kabila la Wasukuma kwenye Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania. Zao hili la muhogo ulio vundikwa hujulikana kwa jina la mbute ambapo huwa ni muhogo ulio kwisha kumenywa na kukaa kwa muda kwa ajili ya matumizi ya baadae kabla ya kuvundikwa na kuwa mbute maalumu kwa ajili ya chakula.