Mchele
Mchele ni punje za mpunga zilizokobolewa baada ya mavuno na kabla ya kupika.
Kama hazijakobolewa na ziko bado katika ganda ni mpunga. Kama zimepikwa huitwa wali.
Watu wengi hununua mchele dukani. Ni punje kavu kabisa zinazokaa muda mrefu hata mwaka bila kuharibika kama hakuna unyevu wala wadudu.
Penye kilimo cha mpunga watu wananunua pia magunia wakikoboa kiasi kile wanachohitaji kwa kipindi.
Mpunga una faida hauathiriki sana na wadudu, lakini mchele uko hatarini kuliwa.
Mchele uliovunjika huuzwa bei nafuu.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |