Shashi
(Elekezwa kutoka Mdondoakupe)
Shashi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 2:
|
Shashi au wadondoakupe ni ndege wadogo kiasi wa jenasi Buphagus, jenasi pekee katika familia Buphagidae. Wanatokea Afrika tu. Ndege hawa wana rangi ya kijivu au kahawa juu na nyeupe au njano kahawia chini. Hula kupe na vidusia wengine kwa ngozi ya wanyama pori wakubwa na ya ng'ombe pia. Hula vidusia vilvyojaa damu hasa na pia damu na tishu za wenyeji. Kwa hivyo wanasababisha vidonda viendelee kuwa wazi na tunaweza kusema kwamba shashi wenyewe ni vidusia. Huliweka tago lao kwa tundu mtini au pengine ukutani. Jike huyataga mayai 2-5.
Spishi
hariri- Buphagus africanus, Shashi Domo-njano (Yellow-billed Oxpecker)
- Buphagus erythrorhynchus, Shashi Domo-jekundu (Red-billed Oxpecker)
Picha
hariri-
Shashi domo-jekundu