Mdudu Mabawa-marefu
Mdudu mabawa-marefu | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nzi-ning'inia wa Kimmins (Bittacus kimminsi) katika Afrika Kusini
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Familia 9:
|
Wadudu mabawa-marefu ni wadudu wadogo wa oda Mecoptera (mèkos = urefu, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Familia muhimu za oda hii ni Panorpidae (nzi-nge) na Bittacidae (nzi-ning'inia).
Mabawa ya wadudu hawa ni membamba na marefu yenye vena nyingi zinazoikizika, kama yale ya wadudu siku-moja. Jenasi kadhaa zina mabawa madogo sana au zimepoteza mabawa kabisa.
Mwili vilevile ni mwembamba na mrefu. Fumbatio ya madume inafanana na mkia wa nge: imepindika juu na ncha yake ina umbo lililopapulika ambalo lina uchi wa kiume ndani yake.
Sehemu za kinywa za wadudu hawa ni sahili. Mandibuli ni ndefu zenye pedipalpi nene. Hukamata arithropodi wadogo au hula mizoga.
Lava wa wadudu mabawa-marefu wanafanana na viwavi wenye miguu sita mifupi ya kweli na miguu kadhaa ya bandia. Pingili ya kumi inabeba kisahani cha mfyonzo au jozi ya vikulabu. Hula maada ya mimea au wadudu waliokufa, pengine hukamata wadudu. Lava hugeuka kwa bundo katika udongo au ubao unaooza.
Picha
hariri-
Bittacidae (Bittacus banksi)
-
Boreidae (Boreus hyemalis)
-
Choristidae (Chorista australis)
-
Eomeropidae (Notiothauma reedi)
-
Meropeidae (Merope tuber)
-
Panorpidae (Panorpa germanica)
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mabawa-marefu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |