Melekeok

Melekeok ni mji mkuu wa nchi ya visiwani ya Palau katika Pasifiki pia mkoa mojawapo wa nchi. Iko kisiwani Babeldaob ambacho ni kisiwa kikubwa cha Palau.

Ramani ya Melekeok
Ziwa la Ngardok

Eneo la mkoa wote wa mji mkuu ni kilomita za mraba 25 na idadi ya wakazi ni 391 (mwaka 2005). Pamoja na Melekeok kuna vijiji saba mkoani.

  1. Melekeok
  2. Ertong
  3. Ngeburch
  4. Ngeremecheluch
  5. Ngermelech
  6. Ngerubesang
  7. Ngeruling

Karibu na mji kuna ziwa la Ngardok lenye eneo la maji la hektari 492.

Melekeok imekuwa mji mkuu tangu Oktoba 2006.


Viungo vya NjeEdit


7°29′36″N 134°38′03″E / 7.49333°N 134.63417°E / 7.49333; 134.63417