Palau (kwa Kipalau: Belau) ni nchi ya visiwani ya Mikronesia katika Bahari ya Pasifiki. Iko takriban km 500 upande wa mashariki wa Ufilipino.

Palau


Ramani ya Palau

Jumla kuna visiwa 250 hadi 350: idadi inategemea namna gani mtazamaji anapendelea kuhesabu sehemu ya nchi kavu kuwa kisiwa kufuatana na ukubwa au udogo wake. Visiwa tisa vimekaliwa na watu na kisiwa kikubwa chenye km² 331 ni Babelthuap.

Hadi mwaka 1994 ilikuwa nchi lindwa chini ya Marekani kwa niaba ya Umoja wa Mataifa. Marekani inaendelea kuwajibika kwa mambo ya kijeshi kufuatana na mkataba uliofanywa baada ya uhuru.

Mji mkuu ni Melekeok kwenye kisiwa cha Babelthuap.

Wakazi ni 18,000 hivi, ambao 65.2% ni wenyeji wenye asili mchanganyiko kutoka visiwa vya Pasifiki, na 31.6% wametokea Asia, hasa Ufilipino.

Kuna lugha tano ambazo huzungumzwa nchini Palau. Lugha rasmi ni Kipalau na Kiingereza.

Upande wa dini, 78.7% ni Wakristo (46.9% ni Wakatoliki, 25.9% Waprotestanti mbali ya 5% ambao ni Waadventista Wasabato). 5.1% wanafuata dini ya Modekngei ambayo inachanganya Ukristo na dini ya jadi. 4.9% ni Waislamu.

Mikoa 16 ya Palau

Tazama pia hariri


  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.