Memorare ("Kumbuka") ni sala ya Wakatoliki kwa Bikira Maria ili kupata maombezi yake.[1]

Kimbilio la wakosefu.

Ingawa mara nyingi Bernardo wa Clairvaux alitajwa kama mtunzi wake[2], kwa mara ya kwanza ilipatikana katika sala ndefu zaidi ya karne ya 15, "Ad sanctitatis tuae pedes, dulcissima Virgo Maria."

Sala ilivyo sasa kwa Kilatini hariri

Memorare, O piissima Virgo Maria,
a saeculo non esse auditum, quemquam ad tua currentem praesidia,
tua implorantem auxilia, tua petentem suffragia,
esse derelictum.
Ego tali animatus confidentia,
ad te, Virgo Virginum, Mater, curro,
ad te venio, coram te gemens peccator assisto.
Noli, Mater Verbi,
verba mea despicere;
sed audi propitia et exaudi.
Amen.

Tafsiri ya Kiswahili hariri

Kumbuka, ee Bikira Maria mwenye rehema,
haijasikika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako,
akiomba shime kwako, akitaka umwombee.
Nami kwa matumaini hayo,
nakukimbilia, ee Mama, mkuu wa mabikira;
ninakuja kwako, nasimama mbele yako
nikilalamika mimi mkosefu,
ewe Mama wa Neno wa Mungu,
usiyakatae maneno yangu,
bali uyasikilize kwa wema, na unitumizie.
Amina.

[3]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Catholic Prayerbook: From Downside Abbey by David Foster 2001 ISBN|0-567-08669-0 page 153
  2. Memorare, from the Latin "Remember", is frequently misattributed to the 12th-century Cistercian monk Saint Bernard of Clairvaux, apparently due to confusion with its 17th-century popularizer, Father Claude Bernard, who stated that he learned it from his own father.
  3. Misale ya waamini, uk. 1525

Viungo vya nje hariri