Sala
Sala (kutoka neno la Kiarabu صلاة, ṣalāh; pia maombi) ni njia ambayo binadamu anauelekea ulimwengu wa roho, hasa kwa nia ya kuongea na Mungu kwa sauti au kimoyomoyo.
Malengo yake yanaweza kuwa tofauti: kusifu, kushukuru, kuomba au kujiachilia.
Upande wa pili sala ni kutafakari ili kusikiliza na kuelewa ujumbe wa Mungu.
Sala inaweza kufanywa na mtu peke yake au na wengi pamoja, hata kwa kuimba.
Sala katika dini mbalimbali
Dini zinaelekeza waumini wake kusali kwa namna mbalimbali.
- Katika Ukristo inaheshimiwa sana liturujia ya mara kwa mara, lakini pia sala ya moyo.
- Uislamu unatofautisha sala, pia swala inayofuata utaratibu maalum na dua ambayo si namna huru ya kumwomba Mungu. Katika Uislamu sala inatakiwa mara 5 kwa siku. Dua ni sala za hiari. Zulia inatumika kwa ajili ya kumsujudia Mungu.
Katika Kanisa Katoliki
Kanisa Katoliki lina maombi bayana sana ambayo wote walioko kanisani husali kwa pamoja. Maombi hayo hufunzwa kwa wote wanaoshiriki kanisani tangu wakiwa wachanga ili waweze kuiga wazee wao. Maombi hayo ni kama majibu ya Misa, rosari, maombi ya waumini, maombi ya toba na kujuta dhambi. Ni lazima Mkatoliki ajue vizuri sala hizo ili ashiriki kikamilifu ibada za Kikatoliki na kuamini katika Ukristo[1].
Katika Uislamu
Sala inayotakiwa kutolewa na kila Mwislamu mara tano kwa siku hufuata utaratibu ufuatao kadri ya utaratibu wa Uislamu wa Kisunn[2]i:
1. Kutia nia 2. Kusimama katika swala ya faradhi pamoja na kuweza 3. Takbiri ya kufungia Swala 4. Kusoma Fatiha 5. Kurukuu 6. Kuitadili kwa kulingana sawa baada ya kurukuu 7. Kusujudu kwa viungo saba 8. Kukaa baina ya sijida mbili 9. Kukaa kwa Atahiyatu ya mwisho. 10. Kusoma Atahiyatu 11. Kumswalia Mtume ﷺ katika Atahiyatu ya mwisho. 12. Kutoa salamu 13. Kujituliza katika nguzo zote 14. Kutungamanisha baina ya nguzo
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiversity has learning materials about Sala |
- media kuhusu Prayer pa Wikimedia Commons
- http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2006/03/23/AR2006032302177.html/ Utafiti kuhusu sala na tiba
- https://www.al-feqh.com/sw chanzo cha fiqhi ya ibada yenye picha zilizochorwa
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sala kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |