Messaoud Bellemou

Mwanamuziki wa Algeria

Messaoud Bellemou, ni mwanamuziki wa nchini Algeria na mmoja wa waigizaji mashuhuri wa muziki wa kisasa wa raï .

Messaoud alianza kazi yake ya kupiga tarumbeta lakini hivi karibuni amejulikana zaidi kwa kuongeza upigaji wa ala za kigeni kama vile saksafoni, [1] violin, na accordion.

Anazingatiwa sana na watu wengine kama mmoja wa baba wa muziki wa kisasa wa Raï,. [2] Mwimbaji wa raï wa Algeri Boutaïaba Sghir alitangaza kuwa ushiriki wa Bellemou katika muziki wa raï ulikuwa muhimu lakini muziki wa raï ulikuwepo kabla ya kuja kwa Bellemou

Mpiga tarumbeta huyu amefanya kazi mnamo mwaka 1970 na waimbaji tofautitofauti wa muziki wa raï wa kizazi chake kama Boutaïaba Sghir, Boussouar El Maghnaoui, Bouteldja Belkacem.

Mnamo miaka ya 1980 neno pop-raï limetumika kuelezea kizazi kipya cha chebs na chebats kutambulisha ala mpya, [3] na pamoja na Belkacem Bouteldja walitoa rekodi ya muziki wa kwanza wa aina hiyo mpya.

Marejeo

hariri
  1. Mehdid, Malika (2006), "For a Song – Censure in Algerian Rai Music", katika Drewett, Michael; Cloonan, Martin (whr.), Popular music censorship in Africa, Ashgate Publishing, uk. 206, ISBN 978-0-7546-5291-5
  2. Cliff Furnald, RootsWorld: African Archive #8, iliwekwa mnamo 2009-03-31
  3. Marranci, Gabriele (2005), "Algerian Raï into Beur Raï: The Music of Return", katika Cooper, David; Dawe, Kevin (whr.), The Mediterranean in Music, Scarecrow Press, uk. 199, ISBN 978-0-8108-5407-9
  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Messaoud Bellemou kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.