Mfereji wa Panama
Mfereji wa Panama ni njia ya maji nchini Panama (Amerika ya Kati) kati ya Bahari ya Pasifiki na Bahari ya Atlantiki. Shingo ya nchi la Panama ni njia fupi kati ya bahari zote mbili.
Kabla ya kujengwa kwa mfereji huu meli zote zilipaswa kuvuka ncha ya kusini ya Amerika na mfereji umefupisha safari hii kwa kilomita maelfu.
Utangulizi wa mfereji ulikuwa reli kutoka Colon upande wa Karibi kwenda mji wa Panama upande wa Pasifiki iliyojengwa 1855. Reli hii ilirahisisha safari kati ya Atlantiki na Pasifiki kwa watu na bidhaa vilivyoelekea watu ule kwenda Kalifornia. Watu wengi walikwenda Kalifornia miaka ile kwa sababu ya dhahabu iliyopatikana kule tangu 1848 na hapakuwa na reli kati ya pwani zote mbili za Marekani wakati ule.
Kampuni ya Kifaransa ilianza kujenga mfereji tangu 1880 lakini ilishindwa. Serikali ya Marekani iliendeleza kazi na kumaliza mfereji mwaka 1914.
Marekani ilitawala kanda ya mfereji kuanzia 1904 hadi mwaka 1999 kwa kuikodi kutoka nchi ya Panama. Siku hizi mfereji uko chini ya serikali ya Panama.
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mfereji wa Panama kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |