Miguel de Olivares
Miguel de Olivares (1675 – 1768) alikuwa kasisi na mwanahistoria wa Chile.
Alizaliwa katika mji wa Chillán. Olivares alijiunga na Shirika la Yesu, akawa mmisionari, na kuanzia mwaka wa 1701 alianza kusafiri katika maeneo ya Quillota, Polpaico, Tiltil, Limache, na mengineyo. Kuanzia mwaka 1712 hadi 1720, aliongoza misheni za Nahuelhuapi na Calbuco. Mnamo mwaka wa 1730, alikuwepo mjini Concepción wakati wa tetemeko la ardhi la Julai lililoharibu kabisa mji huo.[1]
Marejeo
hariri- ↑ Jofré, Manuel (2010-09-24). "Diccionario del Canto General de Pablo Neruda". Anales de la Universidad de Chile. 0 (15). doi:10.5354/0365-7779.2003.3409. ISSN 0365-7779.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |